Stop Poverty Final

YPM imehitimisha mashindano ya Stop Poverty Cup Football League huko wilayani Mkinga mkoani Tanga. Mshindano haya yalipambwa na jumbe mbalimbali zikisomeka katika mabango na kuelezewa vizuri na Afisa michezo kwa maendeleo Bwana Francis Kamote. Moja ya jumbe ambazo zilisomeka kwenye mabango ni ujumbe wa kutokomeza ndoa za utotoni na mimba za utotoni ambapo ujumbe huu ulimgusa mgeni rasmi ambae alikua mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya Mkinga.

Akizungunza baada ya kupewa kipaza sauti aliishukuru taasisi ya YPM kwakunzaisha mpango mzuri wa kushirikiana na jamii ya watu wa Mkinga ili kutokomeza umasikini pamoja na changamoto za ndoa za utotoni na mimba za utotoni. Aidha, aliendelea kwa kukiri kwamba changamoto hii ya mimba za utotoni na ndoa za utotoni bado inaendelea kupasua vichwa vya serikali ya Mkinga na watu wenye nia njema yakutokomeza vitendo hivyo na kwamba anaunga mkono juhudi hizi ili kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya kupata elimu.

Baada ya hayo Meneja miradi wa YPM Bwana Peter Jally aliwahakikishia wananchi kwamba taasisi itaendeleza ushirikiano na jamii na serikali kuhakikisha vitendo kama hivyo vinatokomezwa.

YPM has concluded the Stop Poverty Cup Football League tournament at Mkinga district in Tanga region. The competition was adorned with various messages being read on the posters and well explained by the Sports for Development Officer Mr. Francis Kamote.

One of the messages that was read on the posters was a message on the eradication of Child Marriage and Early Pregnancy where the message touched the guest of honor who was a representative of the District Commissioner as well as the Executive Director of Mkinga District Council. Speaking after receiving the microphone, he thanked YPM for developing a good program to work with the Mkinga community to eradicate poverty as well as the challenges of Child Marriage and Early pregnancy.

In addition, he went on to acknowledge that the challenge of Early Pregnancy and Child Marriage still continues to blow the heads of the Mkinga government and people with good intention to eradicate such practices and that he supports these efforts to ensure children get their right to education. After that YPM Program Manager Mr. Peter Jally assured the public that the organisation will continue to work with the community and the government to ensure that such acts are eradicated.

SIGs follow-up and Training

Mnamo mwezi wa Tisa 09 na 10 mwaka huu YPM, iliongozwa na Meneja Miradi na Afisa  wa mpango wa  Kutokomeza Umaskini, Bwana Peter Jally, iliweza kutembelea vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za kifedha vya Handeni na Kabuku (CMGs).

Katika mpango huo, YPM inahakikisha vikundi hivi vinasonga mbele kwa kuvitembela na kutatua changamoto mbalimbali zinazokumba vikundi hivyo. Uongozi kutoka Ofisi ya Vijana wa Waleta Amani umeendesha semina ya ujasiriamali, kusajili vikundi vidogo vya huduma ndogo za kifedha, na kukumbushia kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza  vikundi hivi. Sio hivyo tu, lakini YPM ametembelea kituo cha kompyuta cha Handeni kinachosimamiwa  na vikundi vya Handeni ili kuona  maendeleo yake.

On September 09 and 10 this year, YPM, led by Program Manager and Economic Justice Program Officer, Mr. Peter Jally, was able to visit Handeni and Kabuku Community Microfinance Groups (CMGs). In this ongoing visit, YPM ensures that, these groups move forward to reach their goals.

The officers from the Youth peacemakers Tanzania provided an entrepreneurship training, registration of the Community Microfinance Groups (CMGs), as well as reviewing the rules, regulations and procedures for running these groups. Not only that, but YPM has visited the Handeni computer center run by Handeni Community Microfinance Groups and monitoring its progress.