Entrepreneurship Training

Mkurugenzi wa Tasisi ya Youth Peacemakers Tanzania (YPM) Mch.Godfrey Walalaze ameendesha semina ya ujasiliamali Makorora Mjini Tanga kwalengo lakuwezesha Washarika wa kanisa la Makorora kuona kutumia fursa mbalimbali zinazinazopatikana katika maeneo yao. Katika seminar hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Mtendaji katika mradi wa Bomba la mafuta kutoka Uganda aliweza kueleza fursa mbali mbali zinazotokana na kutekelezwa kwa mradi huo jijini Tanga.


The Director of Youth Peacemakers Tanzania (YPM) Rev. Godfrey Walalaze has conducted an entrepreneurship seminar at Makorora in Tanga with the aim of empowering Makorora church members to see how to use the various opportunities available in their areas. In the seminar, which was also attended by the Executive in the oil Pipeline project from Uganda, he was able to explain the various opportunities arising from the implementation of the project in Tanga.

TCDD General Assembly

Muungano wa Tanzania wa Madeni na Maendeleo (TCDD) ambapo YPM ni mwanachama ilifanya mkutano wa Mwaka mjini Dodoma kujadili masuala yanayohusu madeni na Maendeleo nchini Tanzania. YPM kama mwanachama iliwakilishwa na Meneja Miradi Bw. Peter Jally. Katika muungano huu YPM pia imejitoa kuwezesha jamii kuhusu uwajibikaji wa kijamii hasa katika kuiwezesha jamii kufanya Ukaguzi wa Kijamii katika sekta ya maji mwaka huu hapa Lushoto.

Tanzania Coalition on Debt and Development (TCDD) whereby YPM is a member held Annual meeting in Dodoma to discuss virous issues concerning debt and Development in Tanzania. YPM as the member was represented by Programs Manager Mr. Peter Jally. In this coalition YPM is also committed to empower the community about social accountability specifically on equipping the community to conduct Social Auditing in water sector this year here in Lushoto.

LUSCO Meeting

Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Lushoto(LUSCO) Mch. Godfrey Tahona Walalaze akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. Mkutano huo uliohudhuriwa na mgeni rasmi Mhe. Kalist Lazaro Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Ikupa Mwaisyoge, mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bumbuli wageni waalikwa na wajumbe.

The Chairperson of Lushoto Civil Society Organisation(LUSCO) Rev. Godfrey Tahona Walalaze speaking to the Annual meeting held in Lushoto District Council venue. The meeting was attended by the guest of honor was Hon. Kalist Lazaro the Lushoto District Commissioner , Lushoto Distric Executive Director Hon. Ikupa Mwaisyoge,representative of Bumbuli Council Director amongst other invited guests and members.