Youth Change Summit (YCS)2023

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis amewakumbusha vijana wenye uelewa kuhusu mazingira kutoa elimu hiyo kwa wananchi wa vijijini wasio na uelewa juu ya athari za uharibifu wa mazingira  ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema hayo katika ufunguzi wa Kongamano la vijana la Youth Change Summit linalojadili mada mbalimbali za mabadiliko ya tabia nchi lililo fanyika  kwa siku mbili wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo amesema ni wakati wa vijana wasomi kuipeleka elimu hiyo maeneo ambayo hayafikiki kirahisi ili kujenga uelewa juu ya athari na madhara yatokanayo na uharibifu wa mazingira.

Participants of YCS 2023

Katika hotuba yake pia Mh.Khamis amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa majiko banifu ambayo yanasaidia kupunguza au kuondosha kabisa vitendo vya ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa sambamba na kuhamasisha matumizi ya mkaa mbadala.

Katika hatua nyingine amebainisha Serikali inaendelea na utaratibu wa kupunguza Kodi Katika nishati mbadala ili wananchi waweze kustahimili kwa kila kaya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya Youth PeaceMakeres Tanzania Mch. Godfrey Tahona Walalaze amesema wamelenga kufanya Kongamano hili la Mazingira kwa kulenga Mabadiliko ya tabia Nchi kwakuwa linaathiri maisha ya binadamu kwa ujumla  na wakiamini vijana wanauwezo mzuri wa kubuni njia bora za kukabiliana na chanzo na athari ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa maisha ya Sasa na baadae.

Youth Change Summit (YCS) 2023

Kongamano la vijana la Youth Change Summit linalofanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro linalohusu Mabadiliko ya Tabia

Nchi,Kongamano hili limefunguliwa hii na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis

Washiriki wa YCS 2023

Youth Change Summit

Youth Change Summit

Youth Change Summit 2023, is centred around the theme “Climate Change: Adapting to Climate Change and Enhancing Resilience.” Which will be held in Kuringe Hall Moshi from November 16-17,2023.

Agenda:

The Youth Change Summit will encompass a series of keynote speeches, panel discussions, workshops, and interactive activities designed to empower youth in the following key areas:

  • Embracing Climate Innovation: Pioneering Solutions for a Sustainable Future.
  • Breaking Barriers, Building Resilience: Advancing Gender Equality in Climate Action.
  • Cultivating -a sustainable Workforce: Uniting for green jobs and -a greener Future

04.Elevating Voices, Driving Change: Empowering climate advocacy for a sustainable Tomorrow.

 Youth Change Summit 2023, umejikita kwenye mada “Mabadiliko ya Tabia ya nchi: Kukabiliana mabadiliko ya tabia ya nchi na kuimarisha Ustahimilivu.” Ambao utafanyika katika ukumbi wa Kuringe Moshi kuanzia Novemba 16-17,2023.

Ajenda:

Mkutano wa Youth change summit utajumuisha mfululizo wa hotuba kuu, mijadala ya jopo, warsha, na shughuli shirikishi zilizoundwa ili kuwawezesha vijana katika maeneo muhimu yafuatayo:

01. Kukumbatia ubunifu wa kushulikia changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi: Suluhu za uanzilishi kwa mustakabali endelevu.

02. Kuvunja Vikwazo, Kujenga Ustahimilivu: Kuendeleza Usawa wa Kijinsia katika kuchukua hatua juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi.

03. Kukuza nguvukazi endelevu: Kuungana kwa ajili ya kazi za kijani.

04.Kupaza sauti, kuendesha mabadiliko: Kuwezesha utetezi wa hali ya hewa kwa kesho endelevu.