Mkataba wa Makubaliano Kati ya YPM Tanzania na CHAMAVITA

Youth Peacemakers Tanzania (YPM) na CHAMAVITA wamesaini makubaliano ya ushirikiano wenye lengo la kuhamasisha amani na maendeleo ya jamii nchini Tanzania. Ushirikiano huu utatumia nguvu za mashirika yote mawili ili kukuza utatuzi wa migogoro, kuwawezesha vijana, na kuanzisha miradi ya maendeleo endelevu kote nchini.

YPM Tanzania, inayojulikana kwa juhudi zake za msingi katika ujenzi wa amani na ushirikishaji wa vijana, itafanya kazi kwa karibu na CHAMAVITA, shirika lililo na dhamira ya maendeleo ya jamii na mshikamano wa kijamii, kutekeleza programu na miradi ya pamoja. Programu hizi zitajumuisha warsha za elimu ya amani, mazungumzo ya jamii, na mafunzo ya ujenzi wa uwezo kwa viongozi vijana.

Ushirikiano kati ya mashirika haya mawili unatarajiwa kuwa na athari kubwa kwa jamii za mitaa kwa kuchanganya rasilimali na utaalamu, YPM Tanzania na CHAMAVITA wanakusudia kushughulikia mizizi ya migogoro na kuunda jamii jumuishi na yenye amani zaidi.

Juhudi za pamoja pia zitalenga kuwawezesha vijana kuwa mawakala wa mabadiliko, wakiwa na ujuzi na maarifa yanayohitajika kuongoza juhudi za ujenzi wa amani katika jamii zao. Ushirikiano huu unaonyesha umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha amani na maendeleo endelevu, na mashirika yote mawili yana matumaini kuhusu matokeo chanya yatakayopatikana.

Memorandum of Understanding between YPM Tanzania CHAMAVITA

Youth Peacemakers Tanzania (YPM) and CHAMAVITA have signed an agreement for the collaboration aimed at fostering peace and community development in Tanzania. The partnership will leverage the strengths of both organizations to promote conflict resolution, youth empowerment, and sustainable development initiatives across the country.

YPM Tanzania, known for its grassroots efforts in peace building and youth engagement, will work closely with CHAMAVITA, an organization dedicated to community development and social cohesion, to implement joint programs and initiatives. These programs will include peace education workshops, community dialogues, and capacity-building training for young leaders.

The collaboration between the two organizations is expected to have a significant impact on local communities by combining resources and expertise, YPM Tanzania and CHAMAVITA aim to address the root causes of conflict and create a more inclusive and peaceful society.

The joint efforts will also focus on empowering young people to become agents of change, equipping them with the skills and knowledge needed to lead peace building efforts in their communities. This partnership underscores the importance of collaboration in achieving sustainable peace and development, and both organizations are optimistic about the positive outcomes it will bring.

Environmetal Management Act Review

Environmental Management Act

Youth Peacemakers brought together young people from the Institute of Judicial Administration (IJA), YPM Youth Forum in Moshi who have come from Machame and KCMC health colleges, along with other participants from Iringa health University and Prince Claus Secondary School in Lushoto. These young people had the opportunity to jointly review the Environmental Management Act of 2024 and reconcile the following matters; –

i/ The law is strong in managing the environment

ii/ It has been seen that society still does not understand enough about this law

iii/ There is no effective management of this law in our areas. After analysing this, the young people agreed on two things to work on in the region of Tanga and Kilimanjaro where the first thing is to provide education on the rights and responsibilities of every citizen on environmental care but also to motivate and cooperate with the Government to ensure that this law it is implemented in our communities.

Sheria ya Usimamizi wa Mazingira

Youth Peacemakers iliwaleta kwa pamoja vijana kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), YPM Youth Forum ya Moshi ambao wametoka Vyuo vya afya vya Machame na KCMC,pamoja  na  washiriki wengine waliooka Chuo cha afya cha Iringa na shule ya Sekondari ya  Prince Claus  iliopo Lushoto. Vijana hawa walipata nafasi ya kupitia kwa pamoja Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2024 na kuanisha mambo yafuatayo; –

i/ Sheria ipo imara katika kusimamia mazingira

ii/ Imeonekana jamii bado hainauwelewa wakutosha juu ya sheria hii

iii/Hakuna usimamizi madhubuti wa sheria hii katiaka maeneo yetu.

Baada ya kuchambua haya vijana hao walikubaliana mambo mawili ya kufanyia kazi katika mkoa wa Tanga na Kilimanjaro ambapo jambo la kwanza ni kuotoa elimu juu ya haki na wajibu wa kila raia juu ya utunzaji wa mazingira lakini pia kuhamasiha na kushirikia na Serikali ili kuhakikisha kwamba sheria hii inatekelezwa na kufuatwa katika jamii zetu.

Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika

Mtoto wa Afrika: Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto

Youth Peacemakers Tanzania (YPM) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, wameungana pamoja katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kiwilaya katika kata ya Dule, jimbo la Mlalo, tarehe 16 juni 2024.

Mtoto wa Afrika ni maadhimisho yanayofanyika kila mwaka tarehe 16 Juni, kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini waliouawa tarehe 16 Juni, 1976 kutokana na uwepo wa ubaguzi wa rangi.

Katika harakati za kudai haki zao za kutobaguliwa pamoja na haki nyingine za kibinadamu kama elimu bora kwa watoto wote, watoto hao waliuliwa kikatili, hivyo mnamo mwaka 1990 Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) kwa sasa (AU), walipitisha Azimio la kuwakumbuka watoto hao waliokua na uthubutu wa kupigania haki zao.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto” ikiwa na lengo la kuwakumbusha wazazi, walezi, Serikali na wadau wengine kuzingatia wajibu wetu katika kuimarisha mifumo ya ulinzi na maendeleo ya Mtoto ili aweze kudhibiti changamoto ya ongezeko la vitendo vya ukatili nchini pamoja na kutoa haki sawa kwa watoto wote bila ubaguzi wa aina yoyote.

Child of Africa: Strengthen Protection and Equal Opportunities for Children

Youth Peacemakers Tanzania (YPM), in collaboration with the Lushoto District Council, have joined together in the celebration of the International  African Child day held at the district level at Dule ward, in Mlalo constituency, on June 16, 2024.

International African Child day is an annual commemoration held on June 16, aiming to remember the children of Soweto, South Africa, who were killed on June 16, 1976, due to the existence of racial segregation.

In their struggle to demand their rights against discrimination, as well as other human rights such as quality education for all children, these children were brutally killed. Hence, in 1990, the Organization of African Unity (OAU), now the African Union (AU), passed a resolution to remember these brave children who fought for their rights.

This year’s theme is “Sustainable Development 2030: Strengthen Protection and Equal Opportunities for Children,” with the aim of reminding parents, guardians, the government, and other stakeholders to fulfill our duty in strengthening child protection systems and development. This is to address the increasing challenges of violence against children in the country and to ensure equal rights for all children without any form of discrimination

Kipindi cha Redio kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika

Mjadala Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika

Kuelekea siku ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Youth Peacemakers Tanzania, wameratibu mjadala wa kuielimisha jamii juu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, kwa kuwaalika vijana wanaounda Peace clubs kutoka Chuo cha uongozi wa mahakama IJA pamoja na wanafunzi wa shule za sekondari katika studio za redio ya Utume FM.

Mjadala huo wenye lengo la kuibua changamoto zinazowakabili watoto, ikiwemo unyanyasaji, ndoa za utotoni, mimba za utotoni na ukatili dhidi ya watoto, umelengwa kuikumbusha jamii kutopuuzia au kukaa kimya pindi wanapoona haki za mtoto zinakiukwa.

Jamii ikishirikiana na serikali katika kuibua vitendo viovu vinavyowakumba watoto, itasaidia utekelezaji wa sera ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, yenye lengo la kuhakikisha kila mtoto anapata haki na wajibu stahiki.

Discussion on the Commemoration of the Intenational African Child Day

As we approach the commemoration of the International African Child Day, Youth Peacemakers Tanzania has organized a discussion to educate the community about this important day. They have invited youth from Peace Clubs at the Judicial Leadership Institute (IJA) and students from secondary schools to participate in the discussion at the studios of Utume FM radio.

This discussion aims to highlight the challenges facing children, including abuse, child marriages, teenage pregnancies, and violence against children. The goal is to remind the community not to ignore or remain silent when they witness violations of children’s rights.

By collaborating with the government to expose the evil acts affecting children, the community can contribute to the implementation of the Sustainable Development Goals for 2030, which aim to ensure that every child receives the appropriate rights and responsibilities.