Mjadala Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
Kuelekea siku ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Youth Peacemakers Tanzania, wameratibu mjadala wa kuielimisha jamii juu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, kwa kuwaalika vijana wanaounda Peace clubs kutoka Chuo cha uongozi wa mahakama IJA pamoja na wanafunzi wa shule za sekondari katika studio za redio ya Utume FM.
Mjadala huo wenye lengo la kuibua changamoto zinazowakabili watoto, ikiwemo unyanyasaji, ndoa za utotoni, mimba za utotoni na ukatili dhidi ya watoto, umelengwa kuikumbusha jamii kutopuuzia au kukaa kimya pindi wanapoona haki za mtoto zinakiukwa.
Jamii ikishirikiana na serikali katika kuibua vitendo viovu vinavyowakumba watoto, itasaidia utekelezaji wa sera ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, yenye lengo la kuhakikisha kila mtoto anapata haki na wajibu stahiki.
Discussion on the Commemoration of the Intenational African Child Day
As we approach the commemoration of the International African Child Day, Youth Peacemakers Tanzania has organized a discussion to educate the community about this important day. They have invited youth from Peace Clubs at the Judicial Leadership Institute (IJA) and students from secondary schools to participate in the discussion at the studios of Utume FM radio.
This discussion aims to highlight the challenges facing children, including abuse, child marriages, teenage pregnancies, and violence against children. The goal is to remind the community not to ignore or remain silent when they witness violations of children’s rights.
By collaborating with the government to expose the evil acts affecting children, the community can contribute to the implementation of the Sustainable Development Goals for 2030, which aim to ensure that every child receives the appropriate rights and responsibilities.