Mtoto wa Afrika: Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto
Youth Peacemakers Tanzania (YPM) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, wameungana pamoja katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kiwilaya katika kata ya Dule, jimbo la Mlalo, tarehe 16 juni 2024.
Mtoto wa Afrika ni maadhimisho yanayofanyika kila mwaka tarehe 16 Juni, kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini waliouawa tarehe 16 Juni, 1976 kutokana na uwepo wa ubaguzi wa rangi.
Katika harakati za kudai haki zao za kutobaguliwa pamoja na haki nyingine za kibinadamu kama elimu bora kwa watoto wote, watoto hao waliuliwa kikatili, hivyo mnamo mwaka 1990 Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) kwa sasa (AU), walipitisha Azimio la kuwakumbuka watoto hao waliokua na uthubutu wa kupigania haki zao.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto” ikiwa na lengo la kuwakumbusha wazazi, walezi, Serikali na wadau wengine kuzingatia wajibu wetu katika kuimarisha mifumo ya ulinzi na maendeleo ya Mtoto ili aweze kudhibiti changamoto ya ongezeko la vitendo vya ukatili nchini pamoja na kutoa haki sawa kwa watoto wote bila ubaguzi wa aina yoyote.
Child of Africa: Strengthen Protection and Equal Opportunities for Children
Youth Peacemakers Tanzania (YPM), in collaboration with the Lushoto District Council, have joined together in the celebration of the International African Child day held at the district level at Dule ward, in Mlalo constituency, on June 16, 2024.
International African Child day is an annual commemoration held on June 16, aiming to remember the children of Soweto, South Africa, who were killed on June 16, 1976, due to the existence of racial segregation.
In their struggle to demand their rights against discrimination, as well as other human rights such as quality education for all children, these children were brutally killed. Hence, in 1990, the Organization of African Unity (OAU), now the African Union (AU), passed a resolution to remember these brave children who fought for their rights.
This year’s theme is “Sustainable Development 2030: Strengthen Protection and Equal Opportunities for Children,” with the aim of reminding parents, guardians, the government, and other stakeholders to fulfill our duty in strengthening child protection systems and development. This is to address the increasing challenges of violence against children in the country and to ensure equal rights for all children without any form of discrimination