Semina ya Maendeleo Endelevu ya dunia.
YPM imeendesha semina iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya YPM hapa Lushoto. Semina hiyo ililenga kusaidia vijana kuongeza uelewa juu ya Maendeleo Endelevu ya Dunia. Vijana Arobaini (40) kutoka klub za amani za shule za sekondari za Shambalai na Ubiri walishiriki mafunzo hayo. Mafunzo haya yamelenga kuwajengea vijana uelewa zaidi juu ya Malengo endelevu ya dunia hususani zaidi ni lengo namba 13 ambalo linahusu maswala mazima ya utunzaji wa mazingira somo ambalo lilitolewa na kijana wa kujitolea ndugu.Tahona Godfrey. Somo la pili lilitolewa na Dkt Glory Kimario ambapo alifafanua juu ya lengo namba 5 usawa wa kijinsia na kusisitiza ni kwa jinsi gani vijana wa kike na wa kiume wanaweza kushiriki pamoja katika kuleta maendeleo. AKizungumza na vijana hao Meneja Miradi wa YPM Bwana Peter Jally aliwaasa vijana hao kushiriki kikamilifu katika kutekeleza malengo hayo ya dunia. Aidha, Mkurugenzi wa Taasisi ya YPM Mch. Godfrey Walalaze alipata wasaa wa Kuzungumza na vijana na kuwaeleza juu ya umuhimu wakunyambua kila lengo vizuri na kujua malengo madogomadogo yalioko kwenye kila lengo ili kurahisisha utekelezaji katika vikundi vyao vya amani mashuleni lakini pia hata katika jamii zao.
YPM inapenda kupongeza shule zote zilizoshiriki, walimu na washiriki wote kwa ujumla katika jitihada hizi endelevu za kujenga uelewa na kurahisisha utekelezaji wa Malengo Endelevu ili kuhakikisha hakuna anae achwa nyuma.
Sustainable Development Goals Seminar.
YPM conducted a seminar held at the YPM office grounds here in Lushoto. The seminar aimed at helping young people raise awareness about Sustainable Development Goals (SDGs). Forty (40) young people from Shambalai and Ubiri peace schools’ clubs participated in the training. This training aims to build young people’s understanding of the Sustainable Development Goals and in particular is goal number 13 which deals with the whole issue of environmental protection a session facilitated by a young volunteer Tahona Godfrey. The second session was delivered by Dr. Glory Kimario where she elaborated on goal number 5 gender equality and emphasized on how young women and men can participate together in bringing about development. Speaking to the youth, YPM Program Manager Mr. Peter Jally urged the youth to actively participate in the pursuit of these global goals. In addition, YPM Institute Director Rev. Godfrey Walalaze had the opportunity to talk to young people and explain to them the importance of tackling each goal well and knowing the sub-goals in each goal to facilitate implementation in their peace groups in schools but also in their communities.
YPM would like to appreciate and thanks all schools, teachers and all participants in this ongoing efforts to build awareness and facilitate the implementation of the Sustainable Development Goals to ensure that no one is left behind.