Mnamo mwezi wa Tisa 09 na 10 mwaka huu YPM, iliongozwa na Meneja Miradi na Afisa wa mpango wa Kutokomeza Umaskini, Bwana Peter Jally, iliweza kutembelea vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za kifedha vya Handeni na Kabuku (CMGs).
Katika mpango huo, YPM inahakikisha vikundi hivi vinasonga mbele kwa kuvitembela na kutatua changamoto mbalimbali zinazokumba vikundi hivyo. Uongozi kutoka Ofisi ya Vijana wa Waleta Amani umeendesha semina ya ujasiriamali, kusajili vikundi vidogo vya huduma ndogo za kifedha, na kukumbushia kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza vikundi hivi. Sio hivyo tu, lakini YPM ametembelea kituo cha kompyuta cha Handeni kinachosimamiwa na vikundi vya Handeni ili kuona maendeleo yake.
On September 09 and 10 this year, YPM, led by Program Manager and Economic Justice Program Officer, Mr. Peter Jally, was able to visit Handeni and Kabuku Community Microfinance Groups (CMGs). In this ongoing visit, YPM ensures that, these groups move forward to reach their goals.
The officers from the Youth peacemakers Tanzania provided an entrepreneurship training, registration of the Community Microfinance Groups (CMGs), as well as reviewing the rules, regulations and procedures for running these groups. Not only that, but YPM has visited the Handeni computer center run by Handeni Community Microfinance Groups and monitoring its progress.