The International Youth Day

                                    MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA KIMATAIFA

Siku ya vijana duniani ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1999 na kuidhinishwa mwaka 2000. Lengo la siku hii ni kuhamasisha uangalizi wa masuala ya kitamaduni na kisheria yanayowahusu vijana.Siku ya vijana duniani huadhimishwa kila mwaka. Tarehe 12 ya mwezi wa 8 imeidhinishwa kama fursa kwa serikali na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali kuwaleta vijana pamoja na kuwaongoza waweze kujadili mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa Maisha yao. Maadhimisho haya huambatana na matamasha, warsha, hafla za kitamaduni, na mikutano ambayo hufanyika ulimwenguni kote nakuhusisha maafisa wa serikali kitaifa, serikali za mitaa na mashirika ya vijana.

Taasisi ya Youth peacemakers (YPM) huadhimisha kuzaliwa kwake tarehe 12 ya mwezi wa 8 kila mwaka sambamba na maadhimisho ya siku ya vijana duniani.  Katika sherehe ya kuadhimisha siku ya vijana duniani taasisi ya Youth Peace Makers iliandaa kongamano la vijana tarehe 14.08 lenye kauli mbiu ya “UIMARISHAJI WA MIFUMO YA CHAKULA KATIKA UKUAJI WA AFYA YA AKILI NA MWILI KWA VIJANA” ikiwa ni kilele cha siku hiyo ya vijana kimataifa kwa taasisi. Kongamano hilo lililohudhuriwa na vijana kutoka shule mbalimbali za sekondari zilizopo katika wilaya ya Lushoto Kama vile Shambalai, Lushoto,Ubiri na Prince Claus. Lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha vijana kutumia vyakula vya asili katika ukuaji wa afya ya akili na mwili. Vijana hao walipata fursa ya kuwasilisha mada mbalimbali kwa njia ya maigizo, nyimbo na ushauri. Zifuatazo ni mada zilizo wasilishwa;

Umuhimu wa chakula mashuleni,Mada hii iliwasilishwa kwa njia ya igizo na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Shambalai, ikionesha umuhimu wa wanafunzi kupata chakula wawapo mashuleni ili kuongeza ufanisisi wa wanafunzi katika masomo yao.

Kushuka kwa uzalishaji wa mazao kipindi cha uviko-19, Mada hii iliwasilishwa na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Prince Claus ikionesha namna ambavyo Uviko-19 ulivyoathiri uzalishaji wa mazao ya chakula kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kwa ujumla.

Kujikinga na Uviko-19, Mada hii iliwasilishwa kwanjia ya wimbo na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Lushoto, wakizungumzia zaidi vijana kujikinga na ugonjwa hatari wa Uviko-19 ili kutunza na kuendeleza nguvu kazi ya taifa.

Umuhimu wa kula vya asili,Mada hii iliwasilishwa kwa njia ya igizo na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Ubiri, ikionesha umuhimu wa matumizi sahihi ya vyakula. Matumizi ya kupindukia ya vyakula vitokavyo viwandani na vyakula vyenye mafuta mengi huathiri afya zetu kwa kiasi kikubwa pia hupelekea vifo kwasababu ya kemikali zitumikazo katika usindikaji wa vyakula hivyo.

                                                         The International Youth Day

World Youth Day was established by the United Nations in 1999 and was approved in 2000. The purpose of the day is to encourage the form of cultural and legal issues related to young people. World Youth Day is celebrated annually and 12th Aug is approved as opportunities for government and non-governmental orgaisations to bring young people together and guide them to discuss various issues that affect their lives. The celebrations involve concerts, workshops, cultural occasions, meetings and discussions to mention a few that are being conducted worldwide and usually attended by young people, elderly people, government officials, local authorities, youth-based organisations and community members at large.

YPM as one of youth-based organisation Tanzania which luckily got its registration on very 12th of Aug 2014 celebrated the day by gathering together young people at her head offices in Lushoto. Youth Peacemakers celebrated the International Youth Day by considering the theme of the day which is “CONSOLIDATION OF FOOD SYSTEMS IN MENTAL AND BODY HEALTH GROWTH FOR YOUNG PEOPLE” where by different government speakers, school students and volunteers cemented their discussion and presentation according to the theme.

The purpose of the event was to encourage young people to use natural foods for mental and body health growth. The young people had the opportunity to present various topics through drama and songs. The following topics were presented by different speakers during the gathering as follows;

The importance of food in School, this topic was presented through the drama by the students from Shambalai Secondary School, showing the importance of pupils to get food in schools so as to increase the activeness of their mind during studies hours.                                                                                                                   The decline in crop production duringCovid-19, This was presented by the students from Prince Claus Secondary school, showing how covid-19 affected food production from the family level to the nation level.                                                                                                                                                                    Fighting against Covid-19, this was presented through song by the students from Lushoto secondary school, leaving young people with a good message of protecting themselves from the risk of covid-19 so as to maintain and develop the national man power.                                                                                                       The importance of natural foods, this topic was presented through the drama by students from Ubiri secondary school, indicating the importance of maintaining proper eating habits. The students stressed that the excessive use of processed foods may affect young health largely, also it can cause diseases like cancer which might lead to deaths.

Finally, YPM presents gratitude to the Lushoto District Executive Director Miss. Ikupa Mwasyoge, the Lushoto District Educational officer at Primary School level, Shambalai, Lushoto, Ubiri and Prince Claus secondary school students who attended the event.