Kila tarehe 5Juni tunaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Pengine, nitakuwa mbinafsi ikiwa sitasema chochote katika siku hii maalum ya kulinda dunia yetu. Lakini cha muhimu zaidi hapa ni kwamba, sisi kama raia wa dunia tunahitaji kubadili mitazamo, tabia mbaya na kuendeleza tabia chanya katika kulinda na kuhifadhi mazingira yetu kwa Maendeleo Endelevu. TAFADHALI FANYA KITU LEO. Vijana wa Peace Makers Tanzania katika siku hii walisherehekea pamoja na wapenda amani kutoka shule ya sekondari ya Shamabalai ambapo siku hiyo ilianza kwa mafunzo kuhusu SDGs yenye kuzingatia kuchukua hatua juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na Usawa wa Kijinsia kwa kuzingatia kwamba, hatua juu ya hali ya hewa inahitaji kila mtu bila kujali jinsia yake au asili yake ya kihistoria. Mafunzo hayo yalifuatiwa na upandaji miti na kisha kukamilika kwa mechi ya mpira wa wavu.

Ninapendekeza utoe maoni yako hapa kile utakachofanya kwa mazingira yako ikiwa ni kweli unataka kubadilisha ulimwengu kama mwanaharakati wa mazingira.

On every 5th of June we celebrate the World Environmental Day. Probably, I would be selfish if I will not say anything in this very special day of protecting our mother earth. But what is more important here is that, we as the global citizens we need to change our bad attitudes, behaviours and develop positive behaviours in protecting and preserving our environment for Sustainable Development. PLEASE DO SOMETHING TODAY.

Youth Peace Makers Tanzania in this day celebrated with peacemakers from Shamabalai secondary school where the day started with a training on SDGs focusing on Climate Action and gender equality to the respect that Climate Action needs everyone regardless of their gender or historic background. The training was followed by trees planting and then finalised by volleyball match.

I kindly argue you comment here what you are going to do for your surroundings if it is real you want to change the world as an environmental activist.