Kwamasimba Stop Poverty Cup ‘Football League”

Mashindano ya Kwamasiba Stop Poverty Cup  ‘Football League’’ yamemaliza kwa mchezo wa finali kati ya Kwamasimba na Mtonga ambapo timu ya mpira wa miguu ya Mtonga ilishinda mechi hiyo kwa mikwaju ya penati.Mashindando hayo yalianzishwa kwaajili ya kuwawezesha vijana kupigana na Umaskini lakini pia kuleta amani, furaha na mshikamano katika jamii. Kulikua na jumbe mbalimbali zilizokua zinapamba mashindano hayo kwaajili ya kuelimisha jamii. Kupiga vita ndoa za utotoni, kuchangamkia fursa za mikopo kutoka halimashari pamoja na kuinua vijana kimichezo kwani michezo ni ajira ni moja ya jumbe zilizokua zikionekana kwenye mabango yalikuwepo uwanjani. Zaidi ya hayo, zawadi zilitolewa kwa mshindi wa kwanza, wa pili na watatu. Viongozi mbalimbali wa Serikali waliipongeza taasisi ya YPM kwa kushiriki vizuri katika shughuli zakuleta maendeleo kwenye jamii na kuahidi kutoa ushirikaono wakaribu kwataaasi kila watakapo itembelea jamii yao.

The Kwamasiba Stop Poverty ‘Cup Football League’’ ended with a final match between Kwamasimba and Mtonga where the Mtonga football team won the match on penalties. The tournament was started to enable young people to fight poverty but also to bring peace, happiness and solidarity in society. There were various messages put up decorating the competition for the purpose of educating the community. Fighting child marriage, seizing credit opportunities from the council as well as uplifting young people in sports as sports are jobs is one of the messages that were appearing on the posters on the field. In addition, prizes were awarded to the first, second and third place winners. Various government officials commended the YPM for its active participation in community development activities and pledged to provide co-operation whenever they visit  their community.

Environmental Protection by Planting Trees

Vijana Waleta Amani Tanzania wanapenda kuwakumbusha kuhusiana na swala la Utunzaji Mazingira kwa kupanda miti.Taasisi imetengeneza Vitalu vya Miti Lushoto katika ofisi za YPM na Korogwe maeneo ya Mgombezi. Unachotakiwa kufanya nikufika iliuweze kupata miti hiyo bure kabisa.(Hii ni mahususi Kwa Vikundi vya Kijamii vya Huduma ndogo za Fedha vya Vijana Waleta Amani).

Youth Peace Makers Tanzania would like to remind you about the issue of Environmental Protection by planting trees. The organization had prepared two tree nurseries in Lushoto and Korogwe. All you have to do is come and get your trees for free. (This is very specific to Peace Makers Community Microfinance Groups).

Vikundi vya YPM Vyaanza kutumia CHOMOKA

Shirika la YPM lilikua linaendesha semina mbalimbali katika mkoa wa Tanga kwa Vikundi Vya Kijamii Vya Watoa Huduma Ndogo Za Fedha kuhusiana na mfumo wa utunzaji kumbukumbu kwa njia ya mtandao ujilikanao kwa jina la CHOMOKA. Mfumo huu ni mfumo mzuri ambao unawawezesha wanakikundi kutunza kumbukumbu zao kupitia simu janja. Tunashukuru vikundi vya Kwedeghe vimeupokea vizuri mfumo huu ambapo vikundi kumi vilinunua simu janja na kuanza kuingiza taarifa zao.Tunapenda kuwaomba wana vikundi wengine kujiunga na mfumo huu ambao utafanya mapinduzi makubwa katika huduma yao na kuwezesha kuondoa changamoto za kimahesabu ambazo zinakumba vikundi hivyo.

YPM has been conducting various seminars in the Tanga region for Community Microfinance Groups related to the online record keeping system called CHOMOKA. This system is a great system that enables group members to keep their records via smart phones. We are grateful that the Kwedeghe groups have received this initiative well where ten groups bought smart phones and started to enter their information. The organization argues all other groups to use this system which will help them to avoid financial challenges that they are encountering.

Notice of death of YPM board member

Youth Peace Makers Tanzania (YPM) is deeply saddened by the loss of its beloved brother David L. Mkami. Mr Mkami was a longtime member of the YPM board. YPM recognizes the great contribution of Mr Mkami in advising to ensure that the organization works well to achieve its goals. YPM extends its condolences to the family of the deceased brother, the leaders and members of the YPM board, YPM staff as well as relatives and friends. The Lord has given and the Lord has taken let his name be glorified.

Rest in peace brother David L. Mkami.

Shirika la Youth Peace Makers Tanzania (YPM) limepata simanzi na majonzi kubwa ya kuondokewa na mpedwa wake ndugu David L. Mkami. Ndugu Mkami alikua mjumbe wa bodi ya YPM kwa muda mrefu. YPM inautambua mchango mkubwa wa ndugu Mkami katika kushauri ili kuhakikisha shirika linafanya kazi vizuri ili kufikia malengo yake. YPM inatoa pole kwa familia ya ndugu mkami, viongozi na wajumbe wa bodi ya YPM, wafanya kazi wa YPM pamoja na ndugu, jamaa na marafiki. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana na lihimidiwe.

Pumzika kwa amani ndugu David L. Mkami.