Shirika la YPM lilikua linaendesha semina mbalimbali katika mkoa wa Tanga kwa Vikundi Vya Kijamii Vya Watoa Huduma Ndogo Za Fedha kuhusiana na mfumo wa utunzaji kumbukumbu kwa njia ya mtandao ujilikanao kwa jina la CHOMOKA. Mfumo huu ni mfumo mzuri ambao unawawezesha wanakikundi kutunza kumbukumbu zao kupitia simu janja. Tunashukuru vikundi vya Kwedeghe vimeupokea vizuri mfumo huu ambapo vikundi kumi vilinunua simu janja na kuanza kuingiza taarifa zao.Tunapenda kuwaomba wana vikundi wengine kujiunga na mfumo huu ambao utafanya mapinduzi makubwa katika huduma yao na kuwezesha kuondoa changamoto za kimahesabu ambazo zinakumba vikundi hivyo.
YPM has been conducting various seminars in the Tanga region for Community Microfinance Groups related to the online record keeping system called CHOMOKA. This system is a great system that enables group members to keep their records via smart phones. We are grateful that the Kwedeghe groups have received this initiative well where ten groups bought smart phones and started to enter their information. The organization argues all other groups to use this system which will help them to avoid financial challenges that they are encountering.