Ufuatiliaji wa maendelea ya Vikundi vya Huduma ndogo za kifedha Handeni (Mailikumi)


Tarehe 27/06/2026, tulifanya ziara muhimu huko Kwemasimba, Handeni (Mailikumi) kwa lengo la kutathmini na kuimarisha maendeleo ya vikundi vya kijamii na kiuchumi. Ziara hii imetoa picha halisi ya mafanikio, changamoto, na hatua zinazohitajika ili kuinua wananchi kiuchumi. 

  1. Kikundi cha Mkombozi
    Kimeanzishwa mwaka 2016, kikiwa na wanachama 44 (Wanaume 2). 
    Kimepiga hatua kubwa kiuchumi kupitia hisa, mikopo, na kina akaunti ya benki (NMB PAMOJA). Wako katika mchakato wa kusajiliwa rasmi na wanafunga mzunguko wao. 
  2. Kikundi cha Amani
    Kimeanza tarehe 04/05/2025, kikiwa na wanachama 15 (Wanawake 13, Wanaume 2). 
    Kinaendelea vizuri na kinajumuisha mfuko wa jamii, huku kikiwa mbioni kufunga mzunguko wake. 

Kikundi cha Juhudi
Kimeanza mwaka 2022, kikiwa na wanachama 24 (Wanawake 18, Wanaume 6). 
Kinajihusisha na mfumo wa hisa na jamii, kikionyesha ari kubwa ya kujikwamua kiuchumi. 
Changamoto Zilizobainishwa
Licha ya mafanikio haya, baadhi ya vikundi vinakabiliwa na changamoto zinazohitaji utatuzi wa haraka, ikiwemo:
Kutorejesha mikopo kwa wakati na mitaji midogo ya biashara. 
Ukosefu wa elimu ya kutosha ya biashara, kilimo, na usimamizi wa muda. 
Baadhi ya vikundi bado havijasajiliwa wala kuwa na akaunti za benki. 


Suluhisho na Pendekezo Letu
Ili kuhakikisha vikundi hivi vinakuwa endelevu na biashara zao hazifi, tunapendekeza na tayari tunaratibu yafuatayo:
Elimu ya Kilimo na Ufugaji: Kuwapatia mafunzo ya vitendo kuhusu ufugaji wa kuku na kilimo cha umwagiliaji cha mazao na mboga mboga. 
Ratiba Maalum: Tayari kuna pendekezo la tarehe 14/11/2026 la kupeleka mtaalamu/mwalimu wa elimu ya ufugaji wa kuku ili kuwajengea uwezo wanachama. 
Ushauri wa Kibiashara: Kuendelea kuvipa elimu ya usimamizi wa fedha, utunzaji wa mitaji, na usajili rasmi wa vikundi vyao.