
Leo, Taasisi ya Youth Peacemakers (YPM) ilitembelea Kituo cha Polisi Wilaya ya Lushoto kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kupitia Dawati la Jinsia na Watoto. Katika ziara hiyo, YPM ilikabidhi kompyuta itakayosaidia kuhifadhi taarifa za kesi za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, ikiwa ni hatua ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa waathirika.

Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi Wilaya ya Lushoto, Afande Melkioli Fundi, aliishukuru YPM kwa mchango huo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana ili kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii. Naye Programs Officer wa Mazingira na Michezo wa YPM, Bw. Kamote Francis, alieleza kuwa YPM itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine katika kujenga jamii salama, yenye usawa na isiyo na ukatili.
Pamoja tunaweza kulinda wanawake na watoto. Kila hatua ina mchango katika kujenga jamii yenye amani na haki kwa wote. 💙
#YouthPeacemakers #YPM #TokomezaUkatiliWaKijinsia #LindaWanawakeNaWatoto #Lushoto #JamiiSalama #GenderEquality
TOGETHER, WE CAN END GENDER-BASED VIOLENCE
Today, Youth Peacemakers (YPM) visited the Lushoto District Police Station to strengthen collaboration in the fight against gender-based violence through the Gender and Children’s Desk.During the visit, YPM donated a computer to support the safe recording and management of gender-based violence cases involving women and children, helping to improve services for survivors.

The Officer Commander of the Criminal Investigation Department (OC-CID) in Lushoto District, Melkioli Fundi, expressed his appreciation to YPM for the valuable contribution and emphasized the importance of continued collaboration in eliminating gender-based violence within the community.Speaking on behalf of YPM,Programs Officer, Mr. Kamote Francis, reaffirmed the organization’s commitment to working closely with the Tanzania Police Force and other stakeholders to build a safer, more inclusive, and violence-free society.
Together, we can protect women and children. Every action counts in building a peaceful, just, and equitable community for all. 💙#YouthPeacemakers #YPM #EndGenderBasedViolence #ProtectWomenAndChildren #Lushoto #SafeCommunities #GenderEquality

