YPM Washiriki Warsha ya Kampeni Kimaendeleo za Vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam

Youth Peacemakers Tanzania (YPM) iliwakilishwa na Afisa wa Mazingira na Michezo, Bw. Francis Kamote pamoja na Salha Daniel, katika warsha ya kampeni za vyombo vya habari iliyoandaliwa na CEFA Tanzania jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo imelenga kujenga uwezo kwa taasisi na vijana kuhusu namna ya kuendesha kampeni zenye ushawishi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

“Ni nafasi nzuri kwa vijana kama sisi kujifunza mbinu bora za kuifikia jamii kwa ujumbe wa maendeleo na uhamasishaji wenye kuleta manufaa katika nchi. Uwezeshaji huu umetufungua macho zaidi juu ya nguvu ya mawasiliano,” alisema Bw. Kamote.

YPM inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhamasisha maendeleo endelevu kupitia sauti za vijana.

YPM Participates in Media Campaign Workshop in Dar es Salaam

Youth Peacemakers Tanzania (YPM) was represented by Mr. Francis Kamote, the Environment and Sports Officer and Salha Daniel at a media campaign workshop organized by CEFA Tanzania in Dar es Salaam.

The workshop aimed to strengthen the capacity of organizations and youth in designing and delivering impactful media and social media campaigns to drive positive change in their communities.

“This was a great opportunity for young people like us to learn effective ways to reach the community with messages of development . This training opened our eyes to the power of communication,” said Mr. Kamote.

YPM remains committed to working with partners to promote sustainable development through the voices of young people.