
Leo, Taasisi ya Youth Peacemakers (YPM) ilitembelea Kituo cha Polisi Wilaya ya Lushoto kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kupitia Dawati la Jinsia na Watoto.
Katika ziara hiyo, YPM ilikabidhi kompyuta itakayosaidia kuhifadhi taarifa za kesi za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, ikiwa ni hatua ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa waathirika.
Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi Wilaya ya Lushoto, Afande Melkioli Fundi, aliishukuru YPM kwa mchango huo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana ili kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.

Naye Programs Officer wa Mazingira na Michezo wa YPM, Bw. Kamote Francis, alieleza kuwa YPM itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine katika kujenga jamii salama, yenye usawa na isiyo na ukatili.
Pamoja tunaweza kulinda wanawake na watoto. Kila hatua ina mchango katika kujenga jamii yenye amani na haki kwa wote.

