Ufuatiliaji wa Maendeleo ya Vikundi vya SIG – Shume na Mziaghembei

Bw. Peter Jally, Meneja wa Miradi kutoka YPM, alifanya ziara ya ufuatiliaji na tathmini katika vijiji vya Shume na Mziaghembei kama sehemu ya juhudi za kuimarisha uendelevu wa vikundi vya vijana na wanawake vinavyosimamiwa na taasisi ya YPM.

Katika ziara hiyo, Bw. Jally alikutana na wanachama wa vikundi vya utoaji wa huduma ndogo za kifedha (SIG – Savings and Investment Groups), ambapo alifuatilia maendeleo yao, changamoto wanazokutana nazo, na kuwasisitiza kufuatilia mchakato wa usajili rasmi wa vikundi hivyo.

Aidha, alitoa elimu ya ujasiriamali pamoja na ushauri wa kitaalamu kuhusu usimamizi bora wa vikundi, ikiwa ni pamoja na utunzaji sahihi wa kumbukumbu na kuhakikisha uwazi katika shughuli zote za vikundi. Pia, aliongoza majadiliano ya pamoja kwa lengo la kutatua changamoto zinazojitokeza ndani ya vikundi hivyo.

Monitoring the Progress of SIG Groups – Shume and Mziaghembei

Mr. Peter Jally, the Project Manager at YPM, conducted a monitoring and evaluation visit in the areas of Shume and Mziaghembei as part of ongoing efforts to strengthen the sustainability of youth and women groups supported by the YPM organization.

During the visit, Mr. Jally met with members of Savings and Investment Groups (SIGs) to assess their progress, understand the challenges they are facing, and emphasized the importance of following up on the formal registration process of these groups.

In addition, Mr. Peter Jally provided entrepreneurship education and professional advice on effective group management, including proper record-keeping and ensuring transparency in all group activities. He also facilitated collective discussions aimed at addressing and resolving challenges arising within the groups.