Mashine ya shughuli za kilimo ya Kikundi cha “Lengo Letu” imefanyiwa marekebisho na sasa ipo tayari kutumika. Kwa marekebisho madogo yaliyosalia, kama kunoa visu, wanakikundi wamejitolea kuyakamilisha kwa kushirikiana.
Mashine hii inawawezesha wakulima kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia kama hatua muhimu kuelekea kilimo cha kisasa. Lengo ni kufanikisha kilimo chenye tija kinacholeta faida kwa wakulima huku kikizingatia utunzaji wa mazingira.
Katika hatua nyingine, semina ya ujasiriamali kuhusu ufugaji wa kuku iliandaliwa kwa wanachama wa vikundi vya VICOBA. Semina hiyo ilifanyika katika ofisi ya Kikundi cha VICOBA cha “Lengo Letu” huko Kijiru, Kata ya Mayomboni. Madhumuni yalikuwa kuwapa wanajamii maarifa ya kujitegemea kiuchumi na kuongeza kipato kwa kuzingatia mbinu bora za ufugaji.
Tunalenga kuimarisha vikundi kupitia elimu na nyenzo bora kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.
#VICOBA #LengoLetu #Ujasiriamali #UfugajiWaKuku #KilimoBora #MaendeleoEndelevu
Lengo Letu Group’s Farm Machine Restored
The agricultural machine of the “Lengo Letu” group has been repaired and is now ready for use. Minor fixes, such as blade sharpening, will be completed by the group members themselves through teamwork.
This machine enables the farmers to embrace technological advancements as a crucial step toward modern farming. The goal is to achieve productive agriculture that benefits the farmers while promoting environmental conservation.
In another development, an entrepreneurship seminar on poultry farming was conducted for members of VICOBA groups. The seminar took place at the office of the “Lengo Letu” VICOBA group in Kijiru, Mayomboni Ward. The objective was to equip the community with skills for economic self-reliance and to boost incomes by adopting effective poultry farming practices.
Our mission remains to strengthen groups through education and practical tools for sustainable economic and social development.
#VICOBA #LengoLetu #Entrepreneurship #PoultryFarming #ModernFarming #SustainableDevelopment