YPM FORUM

Kutana na Youth Peace Makers Forum (YPMF) vijana kutoka Machame Health Institute ambao wanajishughulisha na harakati mbali mbali za kuhakikisha jamii inakuwa salama kimazingira na pia kwenye sekta ya usawa wa kijinsia.Forum hii inajihusisha sana na SDG no 10 Ambayo ni Climate Action pamoja na 17- Reduced inequalities chini ya mwamvuli wa Taasisi ya Youth Peace Tanzania.

Meet Youth Peace Makers Forum(YMPF), these are youth from Machame Health Institute that works hand in hand with Youth Peace Pakers Tanzania to make sure society gets all the help they need specially from the SDG goal no 17&10 that is Climate action and Reduced Inequality. YPM is very proud of this group and appreciate all the work they are doing to make sure the society is safe and gets all the knowledge they deseve.

IJA Peace Club

 IJA Peace Makers

There has been a very productive discussion with 18 youth from the Institute of Judicial Administration (IJA). The purposes were to discuss how the students would be able to collaborate with the YPM, choosing the leadership of the peace club where the Chairperson was elected to be Ms.  Mwanahamisi Sadick the secretary was appointed Mr. Rashid Mdee and the Disciplinary Officer was elected Mr. Josue Felician. Not only that, but the young people discussed how they will address various challenges such as pollution in Lushoto District as well as educate the community on recognizing the laws of Tanzania and becoming good citizens who know their rights and responsibilities. We are grateful that youth are self-aware and actively involved in activities that affect the future of their lives.

Kulikua na mazungumzo mazuri kati ya YPM na vijana 18 kutoka Chuo cha Uongozi  wa Mahakama (IJA). Madhumini yalikua kujadili jinsi wanafunzi  hao watakavyoweza kushirikiana na taasisi ya YPM,Kuchagua uongozi wa peace club ambapo Mwenyekiti alichaguliwa kua Bi. Mwanahamisi Sadick katibu akachaguliwa  Bwn.Rashid Mdee na Mtunza nidhamu alichaguliwa  Bwn. Josue Felician. Sio hivyo tu, bali vijana hao walijadili jinsi watakavyotatua changamoto mbalimbali kama uchafuzi wa mazingira katika Wilaya ya Lushoto pamoja na kuelimisha jamii juu ya kutambua sheria za Tanzania na kua raia wema wanaojua haki na wajibu wao. Tanashukuru kwamba vijana wanajitambua na kushiriki vyema katika shughuli zinazohusu muktakabali wa maisha yao.

Agribusiness

Leo YPM imetembelea wakulima wa viazi mviringo  wa Kwedeghe ambao ni wanavikundi vya kijamii vya  watoa huduma ndogo za kifedha. Dhumuni nikuwaunganisha wakulima hawa na soko ili waweze kuuza zao hili kwa urahisi ambapo YPM imemtafuta mfanya biashara ambaye yupo tayari kununua zao hilo kwa wakulima kwa bei nzuri.

Today YPM has visited the Kwedeghe potatoes growers who are members Community Microfinance Groups. The purpose is to connect these farmers with the market so that they can sell this crop easily. In addition to that, YPM has brought a trader who is willing to buy the potatoes from those farmers in good price.

Mdahalo

Leo taasisi ya YPM ilipata nafasi ya kushiriki katika mdahalo wa mawazo kati ya wanafunzi wa chuo cha mahakama cha IJA (Institute of Judicial Administration) na Chuo cha Ufundi Mabughai -Lushoto Mada ikiwa inasema “Je kuna usawa kati ya jinsia ya kike na jinsia ya kiume katika jamii inayokuzunguka” Upande wa kuunga mkono hoja walikuwa Chuo cha Maendeleo ya jamii na Ufundi na upande wa Kupinga hoja ikiwa ni Chuo Mungu ni mwema vijana wametupa ushirikiano mzuri sana wanachuo wa IJA pamoja na wa Mabughai! Thanks also to YPM crew kwa ushiriki na ushirikiano chanya! *#Youth Peacemakers Tanzania………..together we can!*

Online Meeting

Today Young people from Institute of Judicial Administration (IJA) and other young people around Lushoto town have participated on the online meeting that has been prepared by TIMU/YUNA Tanzania. The topic that was discussed is HEATHY NATIONS WITH YOUTH ON STEERING WHEEL (Realization of GBV Free Society and Reliable SHR for a Sustained Youth Healthy Status)

Kwamasimba Stop Poverty Cup ‘Football League”

Mashindano ya Kwamasiba Stop Poverty Cup  ‘Football League’’ yamemaliza kwa mchezo wa finali kati ya Kwamasimba na Mtonga ambapo timu ya mpira wa miguu ya Mtonga ilishinda mechi hiyo kwa mikwaju ya penati.Mashindando hayo yalianzishwa kwaajili ya kuwawezesha vijana kupigana na Umaskini lakini pia kuleta amani, furaha na mshikamano katika jamii. Kulikua na jumbe mbalimbali zilizokua zinapamba mashindano hayo kwaajili ya kuelimisha jamii. Kupiga vita ndoa za utotoni, kuchangamkia fursa za mikopo kutoka halimashari pamoja na kuinua vijana kimichezo kwani michezo ni ajira ni moja ya jumbe zilizokua zikionekana kwenye mabango yalikuwepo uwanjani. Zaidi ya hayo, zawadi zilitolewa kwa mshindi wa kwanza, wa pili na watatu. Viongozi mbalimbali wa Serikali waliipongeza taasisi ya YPM kwa kushiriki vizuri katika shughuli zakuleta maendeleo kwenye jamii na kuahidi kutoa ushirikaono wakaribu kwataaasi kila watakapo itembelea jamii yao.

The Kwamasiba Stop Poverty ‘Cup Football League’’ ended with a final match between Kwamasimba and Mtonga where the Mtonga football team won the match on penalties. The tournament was started to enable young people to fight poverty but also to bring peace, happiness and solidarity in society. There were various messages put up decorating the competition for the purpose of educating the community. Fighting child marriage, seizing credit opportunities from the council as well as uplifting young people in sports as sports are jobs is one of the messages that were appearing on the posters on the field. In addition, prizes were awarded to the first, second and third place winners. Various government officials commended the YPM for its active participation in community development activities and pledged to provide co-operation whenever they visit  their community.

Environmental Protection by Planting Trees

Vijana Waleta Amani Tanzania wanapenda kuwakumbusha kuhusiana na swala la Utunzaji Mazingira kwa kupanda miti.Taasisi imetengeneza Vitalu vya Miti Lushoto katika ofisi za YPM na Korogwe maeneo ya Mgombezi. Unachotakiwa kufanya nikufika iliuweze kupata miti hiyo bure kabisa.(Hii ni mahususi Kwa Vikundi vya Kijamii vya Huduma ndogo za Fedha vya Vijana Waleta Amani).

Youth Peace Makers Tanzania would like to remind you about the issue of Environmental Protection by planting trees. The organization had prepared two tree nurseries in Lushoto and Korogwe. All you have to do is come and get your trees for free. (This is very specific to Peace Makers Community Microfinance Groups).

Vikundi vya YPM Vyaanza kutumia CHOMOKA

Shirika la YPM lilikua linaendesha semina mbalimbali katika mkoa wa Tanga kwa Vikundi Vya Kijamii Vya Watoa Huduma Ndogo Za Fedha kuhusiana na mfumo wa utunzaji kumbukumbu kwa njia ya mtandao ujilikanao kwa jina la CHOMOKA. Mfumo huu ni mfumo mzuri ambao unawawezesha wanakikundi kutunza kumbukumbu zao kupitia simu janja. Tunashukuru vikundi vya Kwedeghe vimeupokea vizuri mfumo huu ambapo vikundi kumi vilinunua simu janja na kuanza kuingiza taarifa zao.Tunapenda kuwaomba wana vikundi wengine kujiunga na mfumo huu ambao utafanya mapinduzi makubwa katika huduma yao na kuwezesha kuondoa changamoto za kimahesabu ambazo zinakumba vikundi hivyo.

YPM has been conducting various seminars in the Tanga region for Community Microfinance Groups related to the online record keeping system called CHOMOKA. This system is a great system that enables group members to keep their records via smart phones. We are grateful that the Kwedeghe groups have received this initiative well where ten groups bought smart phones and started to enter their information. The organization argues all other groups to use this system which will help them to avoid financial challenges that they are encountering.

Notice of death of YPM board member

Youth Peace Makers Tanzania (YPM) is deeply saddened by the loss of its beloved brother David L. Mkami. Mr Mkami was a longtime member of the YPM board. YPM recognizes the great contribution of Mr Mkami in advising to ensure that the organization works well to achieve its goals. YPM extends its condolences to the family of the deceased brother, the leaders and members of the YPM board, YPM staff as well as relatives and friends. The Lord has given and the Lord has taken let his name be glorified.

Rest in peace brother David L. Mkami.

Shirika la Youth Peace Makers Tanzania (YPM) limepata simanzi na majonzi kubwa ya kuondokewa na mpedwa wake ndugu David L. Mkami. Ndugu Mkami alikua mjumbe wa bodi ya YPM kwa muda mrefu. YPM inautambua mchango mkubwa wa ndugu Mkami katika kushauri ili kuhakikisha shirika linafanya kazi vizuri ili kufikia malengo yake. YPM inatoa pole kwa familia ya ndugu mkami, viongozi na wajumbe wa bodi ya YPM, wafanya kazi wa YPM pamoja na ndugu, jamaa na marafiki. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana na lihimidiwe.

Pumzika kwa amani ndugu David L. Mkami.

The Stop Poverty League at Kwamasimba in Korogwe District

YPM imeanzisha ligi ya mpira wa miguu katika kijiji cha Kwamasimba wilayani Korogwe. Ligi hiyo inaendeshwa kwa jina la ‘Stop Poverty Cup’. Ligi hii imeanzishwa kwa lego la kuinua vipaji vya vijana wa kwamasimba lakini pia kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira,kuzuia ndoa za utotoni, kuelimisha jamii kufuatilia kwa kina juu ya maendeleo yao kupitia serikali, lakini pia na fursa za mikopo ambazo wanaweza kupata katika halimashauri zao.

YPM has established a football league at Kwamasimba village in Korogwe district. The league, known as the ‘Stop Poverty Cup’, has been set up to raise the talents of youth at Kwamasimba but also to educate the community about caring for the environment, preventing child marriage, earl pregnancies, educating the community to make follow-up for their development funds, and credit opportunities that they can get in their councils.