Campaign on Early marriage and Early pregnancy

Tulipata nafasi nzuri ya kukutana na vijana wetu wa klabu ya amani ya YPM katika shule ya sekondari Ubiri. Ilikua ni furaha kuona vijana wanaendelea vyema na shughuli zao za kitaaluma pamoja na kupambana kwaaili ya kudumisha haki na amani katika shule na jamii zao. Kati ya mambo muhimu yaliozungumzwa ni juu ya malengo endelevu ya dunia (SDGs) na kuona ni jinsi gani vijana hao wanaweza kuyafanyia kazi katika shule yao na jamii inayowazunguka.

Sambamba na hilo, wataalamu kutoka YPM walikuza uelewa  wa vijana kuhusu ndoa na mimba za utotoni, na kuwaelimisha vijana hao jinsi ya kupinga na kutokomeza ndoa na mimba za utotoni. Vijana hao waliaswa kwamba, wananafasi kubwa ya  kuwasaidia waliokaribu nao na kuelimisha jamii kutokomeza vitendo hivyo ili kumpa nafasi mtoto wa kike kupata elimu.

Nimatumaini yetu kwamba, wadau mbalimbali watatuunga mkono katika jitihada hizi ili kuwawezesha vijana wetu kupata haki zao za msingi.

We had a great opportunity to meet YPM peace club members at Ubiri secondary School. It was a joy to see young people continue smoothly with their academic activities as well as to fight to maintain justice and peace in their school and communities.

 Amongst the key issues discussed were the Sustainable Development Goals (SDGs) and seeing how these young people can work to contribute on its implementation in their school and the community around them.

 In parallel, experts from YPM raised young people’s awareness of early marriage and pregnancy, and educated them on how to oppose and eliminate early marriage and pregnancy. The young people were persuaded that they had a great opportunity to help those around them and to educate the community to eradicate such practices in order to give the girl a chance to get an education.

 It is our hope that various stakeholders will support us in these efforts to enable our youth to access their basic rights.

visit http://www.norec.no