Safari ya Mafanikio na Maendeleo
Agosti 31, 2024 – Lushoto, Tanga
Youth Peacemakers Tanzania (YPM) imetimiza miaka 10 ya uwepo wake kwa mafanikio makubwa na sherehe za kuvutia zilizofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, Lushoto, Tanga. Tukio hili muhimu lilileta pamoja wanavikundi vya VICOBA, wanafunzi wa Peace Clubs, wawezeshaji wa miradi, pamoja na mgeni rasmi, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, ambaye alitoa hotuba yenye hamasa na kupongeza juhudi za YPM katika kujenga jamii yenye amani na maendeleo.
Maadhimisho haya yalikuwa fursa ya kipekee ya kuangalia safari ya miaka kumi iliyopita, ambayo imejaa changamoto na mafanikio. Mkutano ulianza kwa neno la ukaribisho kutoka kwa Mkurugenzi Mwanzilishi wa YPM, Mchungaji Godfrey Tahona Walalaze, ambaye aliwakumbusha washiriki juu ya maono yaliyoweka msingi wa kuanzishwa kwa YPM: kuwajengea uwezo vijana wa Kitanzania kuwa viongozi wa amani na maendeleo katika jamii zao.
Mhe. Mwanaidi Ali Khamis alitoa hotuba yenye hamasa, akipongeza juhudi za YPM katika kuwawezesha vijana kupitia miradi mbalimbali kama VICOBA na Peace Clubs. Alisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na YPM katika kuboresha maisha ya vijana na jamii kwa ujumla.
Huku tukisherehekea mafanikio ya miaka kumi, YPM inajiandaa kwa miaka mingine kumi ya huduma na maendeleo. Tumepanga kuendelea kuimarisha na kupanua programu zetu ili kuwafikia vijana wengi zaidi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii za Kitanzania. Tutaendelea kushirikiana na wadau wetu, kuhakikisha tunajenga jamii yenye amani, usawa, na maendeleo endelevu.
YPMT inatoa shukrani za dhati kwa washirika, wafadhili wa shughuli (NMB, TIGO na CRDB), , na jamii tunazozitumikia kwa kutuunga mkono katika safari hii. Mafanikio yetu yamejengwa juu ya msingi wa ushirikiano wenu, na kwa pamoja tutaendelea kuleta mabadiliko katika jamii zetu.
Tunatarajia kuona mafanikio zaidi katika miaka ijayo. Endelea kufuatilia habari na taarifa zetu kupitia tovuti na mitandao yetu ya kijamii ili kuona jinsi unavyoweza kushiriki katika kazi zetu.
Youth Peacemakers Tanzania 10th Anniversary Celebration:
A Journey of Success and Growth
August 31, 2024 – Lushoto, Tanga
Youth Peacemakers Tanzania (YPM) celebrated its 10th anniversary with a remarkable event held at Nyerere Square in Lushoto, Tanga. This significant milestone brought together VICOBA group members, Peace Clubs students, project facilitators, and the Guest of Honor, Hon. Mwanaidi Ali Khamis, who delivered an inspiring speech praising YPM’s efforts in building peaceful and prosperous communities.
This anniversary provided a unique opportunity to reflect on the past ten years a journey filled with challenges and achievements. The event commenced with a welcoming address by YPM’s Founding Director, Mchungaji Godfrey Tahona Walalaze, who reminded attendees of the vision that laid the foundation for YPM: to empower Tanzanian youth to become leaders of peace and development within their communities.
Hon. Mwanaidi Ali Khamis delivered a motivating speech, commending YPM’s efforts in empowering youth through various initiatives such as VICOBA and Peace Clubs. She emphasized the importance of continued collaboration with YPM to improve the lives of youth and the broader community.
As we celebrate a decade of success, YPM is preparing for the next ten years of service and development. We plan to continue strengthening and expanding our programs to reach more youth and bring positive change to Tanzanian communities. We will continue to collaborate with our partners to build peaceful, equitable, and sustainable communities.
We would like to express our heartfelt gratitude to our partners, donors (NMB, TIGO, and CRDB), and the communities we serve for supporting us on this journey. Our success has been built on the foundation of your cooperation, and together we will continue to make a difference in our communities.
We look forward to more achievements in the coming years. Stay connected with us through our website and social media platforms to follow our journey and see how you can get involved in our work.