Mkuu wa Mkoa Mh. Batilda Buriani akimvisha medali ya ushindi Moses Kazula mwakilishi kutoka taasisi ya YPM, baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza katika mbio za km5.
Wafanyakazi wa Youth Peacemakers Tanzania (YPM) walishiriki kwenye maonesho ya Usambara Marathon Festival yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, wilayani Lushoto. Maonesho hayo yalivutia idadi kubwa ya washiriki na wadau, yakiwa na lengo la kuhamasisha afya kupitia michezo na kuleta pamoja jamii kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo ya jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Batilda Buriani, alihudhuria na kuongoza maonesho hayo, ambapo alipata fursa ya kuona jitihada mbalimbali zinazofanywa na mashirika kama YPM katika kuhamasisha maendeleo ya vijana na jamii kupitia michezo na shughuli nyingine za kijamii.
YPM ilitumia fursa hii kuonyesha kazi yao ya kipekee katika kuendeleza vijana kupitia mipango ya maendeleo endelevu kama vile uhamasishaji wa amani, mazingira, na michezo kwa maendeleo. Maonyesho haya yameonyesha kwa mara nyingine umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wa michezo na mashirika ya kijamii katika kujenga taifa lenye afya na lenye mafanikio.
Youth Peacemakers Tanzania inaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii kupitia mipango yake ya kijamii na maendeleo.