Mkutano wa Asasi zinazosimamia Ufuatiliaji wa Matumizi ya Rasilimali za Umma
Youth Peacemakers Tanzania imejumuika na asasi mbalimbali za kiraia zinazosimamia utekelezaji wa mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma nchini Tanzania.
Mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao kupitia mtandao wa Zoom, ukijumuisha zaidi ya asasi 153 katika kujadili namna ya kupata muongozo mmoja utakaosimamia mfumo huo wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma.
Mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma ni mfumo unaowekwa na serikali au taasisi husika ili kufuatilia na kudhibiti jinsi rasilimali za umma zinavyotumika. Lengo kuu la mfumo huu ni kuhakikisha uwajibikaji, uwazi, na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma.