Katika juhudi za kina za kutathmini athari zake kwa muongo mmoja uliopita, Youth Peacemakers Tanzania (YPM) imefanya ufuatiliaji wa wiki mbili na makundi ya vikundi vidogo vya kijamii vya huduma ndogo za kifedha (SIGS) ambavyo vinasimamiwa na taasisi. Mpango huu unalenga kutathmini mafanikio na changamoto zinazokabiliwa na makundi haya, kubaini idadi ya vikundi hivyo ambavyo bado vinafanya kazi, na kupima utiifu wao katika ufuatiliaji wa sheria zinazoongoza vikundi hivyo.
Maafisa wa YPM walitembelea maeneo kadhaa yenye vikundi hivyo vya huduma ndogo za kifedha, ikiwemo Mgombezi Korogwe, Konje Handeni, Handeni Mjini, Maili Kumi Handeni, Kwamasimba Korogwe, Kijiru, Kichalikani, na Duga Maforoni huko Mkinga. Makundi haya ya vikundi vidogo vya kijamii vya huduma ndogo za fedha (SIGS) yameonyesha utaratibu mzuri na utiifu wa kufuata sheria zilizowekwa na serikali pamoja na katiba za vikundi vyenyewe, hali iliyochangia mafanikio yao ya kudumu.
Mbali na ufuatiliaji na vikundi hivyo YPM imechukua hatua za kukuza uhamasishaji wa mazingira kwa kutoa semina kwa walimu wa mazingira wa shule za msingi na sekondari za Wilayani Mkinga, zikilenga kuhimiza kampeni za mazingira miongoni mwa wanafunzi. Maafisa pia walitembelea kituo cha mafunzo ya Kompyuta kilichopo Tanga mjini na Wilaya ya Mkinga, vijiji vya Azimio na Tanganyika ili kutambulisha programu za YPM na kutoa ufahamu juu ya dhamira na malengo yake kwa ujumla.
Monitoring and evaluation of small investment groups (SIGS) and Environmental Education Initiatives
In a comprehensive effort to evaluate its impact over the past decade, Youth Peacemakers Tanzania (YPM) has conducted a two-week follow-up with small investments groups (SIGs) managed by the organization. This initiative aims to assess the successes and challenges faced by these groups, determine the number of active SIGs, and measure their adherence to the governing laws and regulations.
YPM officers visited several locations with these Small investments groups, including Mgombezi Korogwe, Konje Handeni, Handeni Mjini, Maili Kumi Handeni, Kwamasimba Korogwe, Kijiru, Kichalikani, and Duga Maforoni in Mkinga. These small investments groups (SIGs) have demonstrated strong organization and adherence to the laws established by the government and the groups’ constitutions, contributing to their sustained success.
In addition to the follow-up with these groups, YPM has taken steps to promote environmental awareness by providing seminars to primary and secondary school environmental teachers in Mkinga District. These seminars aim to encourage environmental campaigns among students. The officers also visited the computer center in Tanga city and Mkinga district, villages of Azimio and Tanganyika to introduce YPM’s programs and provide insights into its overall mission and objectives.