YPM YAENDESHA SEMINA YA SIKU TATU MASHULENI KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA (GBV)

Youth Peacemakers Tanzania (YPM) imeendesha semina ya siku tatu kwa wanafunzi wa shule tatu: Zingibari, Manza, na Kasera, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuelimisha vijana kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia (GBV) na jinsi ya kuutambua, kuuzuia, na kuripoti.

Katika semina hizi, wanafunzi walipata fursa ya kujifunza kwa kina kuhusu aina mbalimbali za ukatili wa kijinsia unaoweza kujitokeza majumbani, mashuleni, na kwenye jamii kwa ujumla. Pia walielimishwa juu ya haki zao, umuhimu wa kutoa taarifa pindi wanapokumbana na vitendo vya ukatili, na namna ya kujenga mazingira salama kwa wote.

Semina hizi zinalenga kuwajengea wanafunzi uelewa wa kutosha ili wawe mabalozi wa mabadiliko na walinzi wa haki za binadamu ndani ya jamii zao.

YPM inaendelea kujitolea katika kulinda haki za watoto na kuhimiza usalama, heshima, na utu kwa wote kupitia elimu ya kijamii.

YPM CONDUCTS THREE-DAY SCHOOL SEMINAR ON GENDER-BASED VIOLENCE (GBV)

Youth Peacemakers Tanzania (YPM) recently conducted a three-day seminar in three secondary schools: Zingibari, Manza, and Kasera, focusing exclusively on the topic of Gender-Based Violence (GBV).

During the sessions, students were equipped with in-depth knowledge about the different forms of GBV that may occur at home, in schools, and within the wider community. They also learned about their rights, the importance of speaking out, and how to report cases of violence safely and effectively.

The seminar aimed to raise awareness and empower students to become change-makers and protectors of human rights within their environments.

YPM remains committed to promoting safety, dignity, and justice for all through education and community engagement.