Youth Peacemakers Tanzania (YPM) imeendesha semina ya ukombozi wa kiuchumi pamoja na masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuwajengea uwezo vijana na akina mama vijana katika maeneo ya haki za kiuchumi, ulinzi wa mtoto na lishe kwaajili ya kudumisha amani endelevu.

Semina ya kwanza ilifanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 6-7 Mei 2025 na ililenga kuwapa vijana elimu juu ya haki za kiuchumi na kuwajengea uelewa wa masuala ya kijamii yanayowahusu, hususani umuhimu wa usawa wa fursa za kiuchumi katika jamii. Mafunzo haya yamewasaidia vijana kutambua nafasi yao katika kujiletea maendeleo na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.
Semina ya pili ilianza tarehe 8-9 Mei 2025 na ilikuwa maalum kwa ajili ya akina mama vijana. Mafunzo haya yaligusia kwa kina masuala ya ukatili wa kijinsia (GBV), malezi ya watoto, lishe bora, na haki za kiuchumi. Washiriki walipata nafasi ya kujifunza mbinu bora za kuwalea watoto wao, kulinda afya zao, na kujitambua kiuchumi ili waweze kujitegemea.

Kupitia semina hizi, YPM inaendelea kuunga mkono jitihada za kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya vijana, kwa kuwapa maarifa na ujuzi muhimu kwa maendeleo yao binafsi na ya jamii zao.
YPM Conducts Economic Justice and GBV Seminars to Empower Youth and Young Mothers
Youth Peacemakers Tanzania (YPM) has successfully conducted economic justice and GBV seminars recently, as part of its ongoing efforts to empower young people and young mothers with knowledge on economic justice, child care, nutrition, and gender issues in Mkinga District.

The first seminar focused on equipping youth with essential knowledge on economic justice and raising their awareness on social issues that affect them. The training helped the youth understand their role in driving change and participating actively in economic and community development.
The second seminars, conducted over two days, were dedicated to young mothers. These sessions addressed key topics such as Gender-Based Violence (GBV), child care, proper nutrition, and economic justice. Participants were trained on how to better care for their children, improve their family health, and become economically independent.

Through these seminars, YPM continues to support the transformation of youth lives by offering relevant knowledge and practical skills to build better futures for themselves and their communities.