Mkutano Mkuu wa Mwaka 2023

Mkutano Mkuu wa Mwaka 2023

Mkutano mkuu wa Taasisi ya YPM Tanzania wenye lengo la kutathmini maendeleo ya taasisi, umefanyika katika ukumbi wa Utondolo tarehe 15 Aprili 2023, ukihudhuriwa na wajumbe, pamoja na wawakilishi wa serikali kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tanga.

Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi ya YPM Tanzania, Mch. Sembuyagi, alifanikiwa kuratibu mkutano huo kwa kusimamia uwasilishwaji wa ripoti mbalimbali ikiwemo, ripoti ya fedha, utekelezaji wa shughuli, mpango kazi wa utekelezaji wa shughuli za YPM pia changamoto na mafanikio yaliyopo katika Taasisi kwa mwaka 2022.

Aidha katibu wa mkutano, amabye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya YPM, Mch. Walalaze alitolea ufafanuzi hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wajumbe kutoka katika ripoti zilizosomwa, ikiwemo suala la umiliki wa ardhi ambalo bado lipo katika hatua za mwisho za makubaliano, ujenzi wa viwanja vya michezo, upatikanaji wa vitega uchumi kwa ajili ya maendeleo ya shirika, Pamoja na uwezeshaji wa vijana.

Akizungumzia sheria ya vikundi vidogo vya uwekaji wa fedha (SIG), Bi. Maria Kakai mwakilishi kutoka ofisi ya maendeleo ya jamii amesema kua, sheria ya sasa ya vikundi hivyo vya fedha vinawataka wanachama kuhakikisha wamesajili vikundi vyao serikalini na pia hawaruhusiwi kuvunja mzunguko wa kikundi kwa kuchukua fedha walizohifadhi ifikapo mwisho wa mwaka na badala yake wanatakiwa kufunga mzunguko kwa kugawana faida kulingana na mzunguko au faida ya kikundi iliyopatikana kulingana na mzunguko au biashara za kikundi na kuendeleza mzunguko wa kikundi.

Youth Peacemakers Tanzania Annual General Meeting 2023

The general meeting of the YPM Tanzania organization with the aim of evaluating the development of the organization, has been held in the Utondolo hall on April 15, 2023, attended by delegates, as well as government representatives from various areas of Tanga region.

The chairman of the meeting who is also the chairman of the Board of YPM Tanzania, Rev. Sembuyagi, managed to coordinate the meeting by managing the presentation of various reports including, financial report, implementation of activities, work plan for the implementation of YPM activities as well as the challenges and achievements in the organization for the year 2022.

In addition, the secretary of the meeting, who is also the Director of the YPM organization, Rev. Walalaze explained the various arguments raised by the members from the reports read, including the issue of land ownership which is still in the final stages of the agreement, the construction of sports grounds, the availability of investments for the development of the organization, along with the facilitation of young people.

Speaking about law and regulation guiding Saving and Investment Group(SIG), Mrs. Maria Kakai, a representative from the community development office, said that the current law of these financial groups requires members to ensure that they have registered their groups with the government, and they are also not allowed to divide shares amongst themselves and starts over again at the end of the group fiscal year and instead they are required to share dividend that was earned at the end of the year.

SIGs Facilitators Training

Mafunzo kwa wawezeshaji wa vikundi vidogo vya kijamii vya huduma ndogo za fedha (SIGs) yamefanyika katika viwanja vya taasisi ya YPM Tanzania kuanzia tarehe 23 hadi 24 mwezi Machi 2023 kwa lengo la kuwakumbusha wawezeshaji mbinu mbalimbali za kuendesha vikundi hivyo.

Meneja wa Taasisi ya YPM Tanzania akiendesha mjadala wa mafunzo ya SIGs kwa wawezeshaji

Akiendesha mjadala uliohusiana na kutambua changamoto na mafanikio yaliyofikiwa na SIGs Rev. Walalaze, Mkurugenzi wa Taasisi ya YPM Tanzania, amewasihi wawezeshaji hao kutembelea vikundi mbalimbali na kufuatilia changamoto wanazopitia na kuwasaidia wanavikundi kutatua changamoto hizo, pia amewasihi wawezeshji kufuatilia mienendo ya vikundi vyote wanavyovisimamia.

Mwezeshaji wa mkutano huo ambaye pia ni Meneja wa YPM Tanzania Bw. Peter Jally amesema kuwa, wawezeshaji wanayonafasi kubwa katika kuhakikisha maendeleo ya vikundi na wanavikundi yanakua ya mafanikio, pia amewasihi wawezeshaji kuhakikisha vikundi havivunji mzunguko bali wanaendeleza mzunguko wa uwekaji wa hisa ili kuweza kumnufaisha mwanakikundi kupata asilimia kubwa ya mkopo na gawio pindi kikundi kinapo funga mzunguko wa mwaka.

Aidha Afisa michezo na utetezi wa mazingira Bw. Francis Kamote amewasihi wawezeshaji kujua namna sahihi ya kuikabili migogoro inayokumba vikundi kwa kutumia busara ili kuepusha uwezekano wa uvunjaji vikundi kwani migogoro midogomidogo ndiyo inayopelekea vikundi vingi kuvunjika.

Bw. Yona James mmoja wa wawezeshaji  anawasishi watu wajiunge na vikundi hivi kwani vinasaidia sana hasa pale mtu anapohitaji mkopo wa haraka, “uwepo wa vikundi hivi vinasaidia sana hasa pale unapopata shida ambayo inahitaji utatuzi wa fedha wa haraka, unakua na uwezo wa kupata mkopo kutoka katika kikundi ulichopo na kwa riba nafuu”.

Akitoa ushauri kwa wakina mama Pamoja na vijana Bi. Melina Mhema, muwezeshaji na mwanakikundi wa vikundi vya Shume na Ufunuo amesema “nawashauri akina mama na vijana kujiunga na vikundi hivi kwani inasaidia kupata mtaji na kujikwamua kiuchumi, mfano mimi nimeweza kujikwamua kutoka katika umasikini kutokana na kujiunga na vikundi na kwa sasa ni mjasiriamali namiliki biashara ya chakula, na nafuga kuku.

Training for YPM SIGs Facilitators

Training for the facilitators of Saving and Investment Groups (SIGs) was held on the grounds of the YPM from the 23rd to the 24th of March 2023 with the aim of reminding the facilitators on the various methods of running those groups.

Rev. Walalaze, the Director of the YPM Tanzania conducted a discussion related to recognizing the challenges and achievements achieved by the SIGs. He urged the facilitators to visit various groups and monitor the challenges they are experiencing and help the group members solve those challenges. He also urged the facilitators to monitor the movements of all the groups they manage.

The facilitator of the meeting, who is also the Manager of YPM Tanzania Mr. Peter Jally, said that the facilitators have a great opportunity to ensure that the development of groups and group members is successful. He also urged the facilitators to ensure that the groups do not take out dividend by the closing of each year, but instead continue stock placement over several years to be able to get a larger percentage of loans and dividends.

In addition, The Sports and Environmental Protection Officer Mr. Francis Kamote urged the facilitators to know conflict resolution and tactics to avoid groups breaking up because of small conflicts, which has been the source of closure of many groups.

Mr. Yona James, one of the facilitators, said that he urges people to join these groups because they are very helpful especially when someone needs a quick loan. “The presence of these groups is very helpful especially when you have a problem that requires a quick financial solution, you are able to get a loan from in the group you are in and at a low interest rate”.

Giving advice to mothers and young people, Mrs. Melina Mhema, a facilitator and group member of the Shume and Ufunuo groups has said “I advise mothers and young people to join these groups because it helps to get capital and fight poverty. For example I have been able to alleviate my personal financial challenges by joining groups and now I am an entrepreneur and I own a business of food, and I raise chickens too, so it’s better”.

Ujasiriamali wa kutengeneza sabuni

Mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo

Bi Ewaldina akitoa mafunzo ya ujasiriamali wa kutengeneza sabuni ya maji katika shule ya sekondari ya Prince Claus

Mafunzo ya ujasiriamali wa kutengeneza sabuni ya maji kwa vitendo yamefanyika tarehe 10 mwezi Machi 2023 katika Shule ya Sekondari ya Prince Claus (SSPC), yakiendeshwa na Bi. Ewaldina Paul kutoka Taasisi ya YPM, kwa lengo la kuhamasisha vijana wadogo kujihusisha na ujasiriamali.

Akitoa mafunzo hayo kwa wanafunzi na baadhi ya walimu waliohudhuria, Bi. Ewaldina amesema “vijana tunapaswa kuwa wabunifu katika kuupiga vita umasikini, na kutokana na upungufu wa ajira tunaweza kuwa wajasiriamali na kujiajiri wenyewe, hivyo leo Taasisi ya YPM Tanzania imeona vyema kuwaletea mafunzo haya ili ikawe chachu kwenu”.

Aidha, Zamana Ibrahimu mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo amesema amefurahishwa na namna taasisi ya YPM ilivyowapa fursa ya kujifunza ujasiriamali, “Taasisi imetuamini sisi kama vijana na tunashukuru kupata fursa ya ujasiriamali hasa kwa sisi tunaomaliza kidato cha nne, ni fursa nzuri na naahidi nitaenda kuitumia fursa hii vizuri”.

“Mafunzo haya yanatupatia fursa sisi wanafunzi kujipatia kipato na pia tutaanza kuzalisha sabuni kwa ajili ya matumizi ya kusafishia maeneo ya shule kama vile vyooni na madarasani, hakika tutawaelekeza na wazazi nyumbani pia ili waweze kutengeneza na kuongeza kipato cha familia” Abdala Saidi mwanafunzi wa kidato cha nne.

Muonakano wa sabuni ya maji baada ya kutengenezwa katika somo la ujasiliamali

Mwalimu Mkuu wa SSPC Richard Onai Shembwana amewashukuru YPM kwa kuwapatia fursa hii na ameahidi kutumia ujuzi huo kuwahafundisha wanafunzi utengenezaji wa sabuni hizo kwa ajili ya matumizi ya shule na nyumbani pia.

Entrepreneurship training on how to make liquid soap was held on March 10, 2023 at Prince Claus Secondary School (SSPC), conducted by Ms. Ewaldina Paul from the YPM Institute, with the aim of encouraging young people to get involved in entrepreneurship.

Giving training to the students and some of the teachers who attended, Ms. Ewaldina said “young people should be creative in fighting poverty, and due to the lack of employment we can be entrepreneurs and self-employed, so today the YPM Tanzania Institute has seen fit to bring you this training so that it becomes a springboard for you”.

In addition, Zamana Ibrahimu a form four student at SSPC, said she was happy with the way YPM institution gave them the opportunity to learn entrepreneurship, “The institution has believed in us as young people and we are grateful to have the opportunity to do entrepreneurship, especially for those of us who are graduating form four, it is a good opportunity and I promise to use this opportunity well”.

“This training gives us the opportunity to earn an income and we will also start producing soap for use in cleaning school areas such as toilets and classrooms. We will also teach our parents and family at home so that it can be a contribution to the family’s income” said Abdala Saidi, a student of the four.

The Principal of SSPC Richard Onai Shembwana thanked YPM for giving them this opportunity and has promised to use that knowledge to teach the students how to make soaps for school and home use as well.

Women Day 2023

Mh. Sekiboko: Wanawake tumieni teknolojia kujiendeleza

Mh. Husna Sekiboko, Mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa Tanga, ambaye ni mgeni rasmi, ameambatana na mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh. Ekalisti Lazaro pamoja na wanawake kutoka taasisi za serikali na zisizo za kiserikali kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Lushoto kufanya maadhimisho ya siku ya Wanawake Kimataifa yaliyoadhimishwa kiwilaya katika Kijiji cha Lunguza kata ya Lunguza tarehe 8 mwezi machi 2023, wakiongozwa na kaulimbiu “Uvumbuzi na maendeleo ya kiteknolojia kwa usawa wa kijinsia”.

Wanawake kutoka taasisi ya Youth Peacemakers Tanzania wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake kimataifa, iliyofanyika katika viwanja vya kata ya Lunguza. Photo by YPM

Mh. Sekiboko amesema wanawake wanapaswa kutumia teknolojia ya mawasiliano kujiendeleza kibiashara na kuwafundisha wanawake wengine mbinu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi kwa kutumia simu za mikononi. Pia amewaasa wazazi kuwaelekeza watoto wao matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kujiendeleza kielimu kuliko kutumia muda mwingi katika kuperuzi tovuti na kurasa zisizo na maadili.

“Wanaume wanapaswa kushirikiana na wanawake katika kulea familia kwa upendo na sio kuwaachia wanawake wenyewe’, amesema Mh. Sekiboko. Halikadhalika amepinga vikali uwepo wa mila potofu ambazo humkandamiza mwanamke kama vile kurithi mke wa marehemu kwani ni mila inayohatarisha usalama wa afya ya mwanamke anayerithiwa.

Upande wa kupinga ukatili wa kijinsia Mh. Sekiboko amesema wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto wao michezo yenye staha, michezo ambayo haitawafanya watu wengine wawatamani watoto kutokana na maumbile, hivyo si vyema mzazi kumruhusu mtoto kunengua mbele za watu ili kumkinga na unyanyasaji wa kijinsia.

YPM Tanzania imeazimisha siku hii kwa kuanza na shughuli mbalimbali za usafi katika eneo la ofisi ya YPM siku ya jumamosi tarehe 4 machi, kisha kufuatia na ugawaji wa taulo za kike katika shule ya Prince Claus, ambako waliambatana na wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, wafanyakazi wa ustawi wa jamii pamoja na redio Utume.

Women should use technology for their own development, Ed. Sekiboko

Hon. Husna Sekiboko, Member of Parliament for CCM special seats in Tanga region, who is an official guest, has accompanied the head of Lushoto District Hon. Ekalisti Lazaro together with women from government and non-government organisation from various parts of Lushoto district to celebrate the International Women’s Day celebrated in the district in Lunguza Village, Lunguza ward on March 8, 2023, and the slogan was “innovation and technology for gender equality”

Hon. Sekiboko said that women should use communication technology to develop themselves commercially and teach other women various ways to get help themselves economically by using mobile phones. She also urged parents to direct their children to the correct use of social networks to help them develop themselves educationally instead of spending a lot of time browsing immoral websites and pages.

“Men should cooperate with women in raising a family with love and not leave it to women themselves”, said Hon. Sekiboko Furthermore, she strongly opposed the existence of stereotypes that oppress women, such as inheriting the wife of the deceased, as it is a tradition that endangers the health of the inherited woman.

On sexual violence issues Hon. Sekiboko said that parents should teach their children decent games, games that will not make other people want to exploit children, so it is not good for a parent to allow a child to play in front of people to protect him from sexual abuse.

Wanawake kutoka YPM Tanzania, Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, na ustawi wa Jamii walijitokeza katika zoezi la ugawaji wa taulo za kike katika shule ya Sekondari ya Prince Claus, kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake kimataifa.

YPM Tanzania has commemorated this day by starting with various cleaning activities in the area of the YPM office on Saturday 4 March, then following with the distribution of female towels (pads) at Prince Claus Secondary School, where they were joined by the staff of the Lushoto District Council, social welfare workers as well as Utume radio workers.

Peace Club Debate

Malumbano ya Hoja

Malumbano ya mdahalo yenye lengo la kukuza matumizi ya lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Shambalai na Ubiri ulifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya shambalia ukiendeshwa na hoja isemayo “chochote anachofanya mwanaume mwanamke anauwezo wa kukifanya vizuri zaidi”

Malumbano hayo ya hoja yalihudhuliwa na taasisi ya youth Peacemakers Tanzania kama sehemu mojawapo ya taasisi kuibua na kusimamia shughuli za kitaaluma katika shule za serikali mkoani Tanga, na pia kuleta chachu ya usawa wa kijinsia kwa wanafunzi kwa lengo la kukuza kizazi chenye utambuzi wa umuhimu wa usawa wa kijinsia katika maendeleo ya jamii nanchi kwa ujumla.

Wanafunzi wa shule zote mbili walitumia fursa hiyo ya mdahalo kuonyesha vipaji mbalimbali kama kucheza, urembo wa asili, ubunifu wa mavazi ambavyo vyote vinamauandaa kijana wa kitanzania kuwa na fani tofauti ambayo itamsaidia katika Maisha. Sanaa ni nyenzo nzuri ya kuwasaidia vijana kuelewa umuhimu wa taaluma pamoja na fani nyingine za sanaa katika kujitengenezea maarifa na kuinua uchumu wa jamii.

Youth Peacemakers Tanzania imekua ikiratibu shughuli za Sanaa, michezo na midahalo katika jamii kama sehemu ya kuwavutia wanafunzi kupenda kusoma na pia kuwa wabunifu katika Sanaa mbalimbali.

………………………

Peace Club Debate

A debate on the intention of promoting the use of English language for Shambalai and Ubiri Secondary School students took place at the Shambalai Secondary School grounds run by the argument that “whatever the man can do a woman can do it better”

The discussion was witnessed by the Youth Peacemakers Tanzania as part of one of the organization plan to develop and manage professional activities in public schools in Tanga, as well as bring leaven to gender equality to students with the aim of promoting a generation with gender equality for community development in general.

Students of both schools took advantage of the debate showing a variety of talents such as dancing, natural beauty, fashion show that aim to prepare a youth to have different professions that would help them in life. Art is a great tool to help young people understand the importance of profession and other arts in developing knowledge and promoting socialism.

Youth Peacemakers Tanzania has been coordinating arts, sports and debates in the community as part of attracting students to learn and also be creative in various arts.

Malumbano ya Hoja

Malumbano ya mdahalo yenye lengo la kukuza matumizi ya lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Shambalai na Ubiri ulifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya shambalia ukiendeshwa na hoja isemayo “chochote anachofanya mwanaume mwanamke anauwezo wa kukifanya vizuri zaidi”

Malumbano hayo ya hoja yalihudhuliwa na taasisi ya youth Peacemakers Tanzania kama sehemu mojawapo ya taasisi kuibua na kusimamia shughuli za kitaaluma katika shule za serikali mkoani Tanga, na pia kuleta chachu ya usawa wa kijinsia kwa wanafunzi kwa lengo la kukuza kizazi chenye utambuzi wa umuhimu wa usawa wa kijinsia katika maendeleo ya jamii nanchi kwa ujumla.

Wanafunzi wa shule zote mbili walitumia fursa hiyo ya mdahalo kuonyesha vipaji mbalimbali kama kucheza, urembo wa asili, ubunifu wa mavazi ambavyo vyote vinamauandaa kijana wa kitanzania kuwa na fani tofauti ambayo itamsaidia katika Maisha. Sanaa ni nyenzo nzuri ya kuwasaidia vijana kuelewa umuhimu wa taaluma pamoja na fani nyingine za sanaa katika kujitengenezea maarifa na kuinua uchumu wa jamii.

Youth Peacemakers Tanzania imekua ikiratibu shughuli za Sanaa, michezo na midahalo katika jamii kama sehemu ya kuwavutia wanafunzi kupenda kusoma na pia kuwa wabunifu katika Sanaa mbalimbali.

………………………

Peace Club Debate

A debate on the intention of promoting the use of English language for Shambalai and Ubiri Secondary School students took place at the Shambalai Secondary School grounds run by the argument that “whatever the man can do a woman can do it better”

The discussion was witnessed by the Youth Peacemakers Tanzania as part of one of the organization plan to develop and manage professional activities in public schools in Tanga, as well as bring leaven to gender equality to students with the aim of promoting a generation with gender equality for community development in general.

Students of both schools took advantage of the debate showing a variety of talents such as dancing, natural beauty, fashion show that aim to prepare a youth to have different professions that would help them in life. Art is a great tool to help young people understand the importance of profession and other arts in developing knowledge and promoting socialism.

Youth Peacemakers Tanzania has been coordinating arts, sports and debates in the community as part of attracting students to learn and also be creative in various arts.

SIGs Monitoring and Evalution 2023

Last week YPM staff visited one of the SIG groups in Ngulwi. The group established in 2021 is moving steadily towards their goals and had already built a sizeable capital amongst themselves. Together, the 31 women raised funds for education, children and social projects. YPMs advocacy officer urged the group to establish a sustainable and safe solution for money saving that secures the rights of all members.

Wiki iliyopita wafanyakazi wa YPM walitembelea moja ya vikundi vya VICOBA huko Ngulwi. Kikundi kilichoanzishwa mwaka wa 2021 kinasonga kwa kasi kuelekea malengo yao na tayari kilikuwa kimejenga mtaji mkubwa miongoni mwao. Kwa pamoja, wanawake 31 walichangisha fedha kwa ajili ya elimu, watoto na miradi ya kijamii. Afisa utetezi wa YPMs alihimiza kikundi kuanzisha suluhisho endelevu na salama la kuokoa pesa ambalo linalinda haki za wanachama wote.

World AIDs Celebration

Say NO TO Early Marriage

Leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani kauli mbiu ya mwaka huu ni IMARISHA USAWA Kauli mbiu hii inasisitiza kuimarisha USAWA katika maeneo yote katika jitihada za kudhibiti UKIMWI kwa hakikisha hakuna vikwazo vya Kiusawa katika jamii hasa usawa wa Kijinsia.

Today is the day of World AIDS Day, this year’s theme is STRENGTHEN EQUALITY This theme emphasizes strengthening EQUALITY in all areas in an effort to control AIDS by making sure there are no barriers to equality in society, especially gender equality.

International Day for Poverty Eradication

Today is the International Day for Poverty Eradication. Youth Peacemakers Tanzania is so humbled to join hands with the rest of the world to see how far we have come across and what are the challenges in this movement of Poverty eradication. Not only that but   also employing new strategies to fight against poverty.

Dignity for all in practice is the umbrella theme of the International Day for the Eradication of Poverty for 2022-2023. The dignity of the human being is not only a fundamental right in itself but constitutes the basis of all other fundamental rights.

Let’s all join together to eradicate Poverty by making the world a better place. It starts with the community around you

Leo ni siku muhimu kwetu kama Taasisi ya Vijana Waleta Amani Tanzania. Siku  hii ni siku ya Kutokomeza Umasikini. Tunanyenyekea na kuunganisha nguvu na wadau wengine ili kuona tulipotoka na tulipo na kuona nijinsi gani Tunaweza kuweka mbinu mpya za Kutokomeza Umasikini.

THE LUNCHING OF “STOP POVERTY CUP’’ FOOTBALL LEAGUE AT EASTERN MLALO DIVISION IN LUSHOTO DISTRICT

THE LUNCHING OF “STOP POVERTY CUP’’ FOOTBALL LEAGUE AT EASTERN MLALO DIVISION IN LUSHOTO DISTRICT

Jana ilikua siku njema kwa wana Msale ambao walikua wamekusanjika katika uwanja wao wa kijii cha Msale katika kata ya Hemtoye kwa shangwe na nderemo wakiwakilisha makundi yote yaliopo kwenye jamii yao ya wazee, watoto, vijana wanawake na watu wenye ulemavu wote kwa pamoja walikuwa tayari kushuhudia mtanange wa kukata na shoka wa ufunguzi wa mashindano ya Ligi ya Mpira wa Miguu katika kampeni ya “kutokomeza umaskini” yajulikanayo kama “Stop Poverty Cup Football League” ambapo zaidi ya timu kumi kutoka katika vijiji na vitongoji mbalimbali  zimethibitisha kushiriki ligi hii. Mechi ya ufunguzi ilihusisha timu ya Nyuki FC toka kijiji cha Msale vs Villa FC kutoka kijiji cha Ziga. Mechi iliisha kwa Nyuki FC kuibuka na ushindi wa goli 4 – 1 dhidi ya Villa FC.

 YPM inaendesha mashindano kama haya katika Wilaya za Mkinga na Korogwe kwa takribani miaka mitano sasa, kulingana na mafanikio yaliopatikana katika mashindano haya yanayolenga kutokomeza umaskini, kudumisha Amani katika jamii, kuhamasisha jamii kupinga ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni pamoja na kuinua jamii kiuchumi kupitia vikundi vya kijasiliamali na kukuza uwelewa juu ya mikopo ya halimashauri inayolenga vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

 Katika kuona mafanikio ya ligi hii YPM iliona vyema kuanzisha mashindano haya ili kuleta chachu ya maendeleo chanya katika Tarafa Mlalo ambapo timu shiriki zimetoka katika kata za Hemtoye.  Kilole. Kwekanga. Malindi na Malibwi. Akizungumza na watu waliokusanyika kushuhudia ufunguzi huo Meneja miradi wa YPM Mr. Peter Jally alisema ‘’Mashindano haya ni kwa ajili ya kuwaleta watu pamoja kuweza kutatua chanamoto mabalimbali zinazoikumba jamiii yao ikiwemo chagamoto za kiuchumi, kijamii kama vile kupinga vitendo viovu vinavyohatarisha Amani katika jamii bila kusahau ukatili wa kijinsia na kupinga ndoa na mimba za utotoni’’. Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa kijiji cha Msale Mh. Amdi Abeid amefurahishwa na ujio wa taasisi ya YPM kwa kuleta mashindano hayo kwa kusema  kuwa “Ni nafasi ya upendeleleo kwao na wanaahidi kuitumia vizuri fursa hiyo ili kusaidia vijana na jamii kuleta maendeleo binafsi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla katika michezo’.

 Hata hivyo Afisa Mazingira na Michezo kwa maendeleo Ndg. Francis Kamote aliwaasa vijana wanaoshiriki mashindano hayo kutumia nafasi walioipata ili kuendeleza vipaji vyao maana michezo ni ajira. Alisisitiza pia utunzaji wa mazingira kwa kuwa ni suala mtambuka kwa kusema ‘’Niwaombe ndugu zangu pamoja na mambo ya michezo ambako huku tunaibua na kuendeleza vipaji na kutengeneza mazingira ya mtu kuajiliwa na kujiajiri kupitia michezo, ni lazima tukumbuke na kusimama imara katika utunzaji wa Mazingira kwakuwa suala hili ni nyeti na ni suala mtambuka. Utunzaji wa Mazingira ni suala ambalo haliepukiki. Maisha ni mazingira na mazingira ni maisha. Tunamshukuru mwenyezi Mungu ambae ametuwezesha kutusimamia na kufanikisha jambo hili’’

THE LAUNCHING OF “STOP POVERTY CUP” FOOTBALL LEAGUE AT EASTERN MLALO DIVISION IN LUSHOTO DISTRICT

Yesterday was a good day for the Msale people who had gathered in their field of Msale village in Hemtoye ward with joy and excitement representing all the groups in their community the elderly, children, young women and people with disabilities were all ready to witness the match of the opening of the Football League competition in the campaign to “eradicate poverty” known as “Stop Poverty Cup Football League” where more than ten teams from various villages and neighbourhoods have confirmed to participate in this league. The opening match involved the Nyuki FC team from Msale village vs Villa FC from Ziga village. The match ended with Nyuki FC winning 4-1 against Villa FC.

 YPM has been conducting such competitions in Mkinga and Korogwe Districts for about five years now, based on the success achieved in these competitions aimed at eradicating poverty, maintaining Peace in the community, mobilizing the community to oppose gender violence,earlys marriage and early pregnancies as well as raising the community economically through entrepreneurial groups and promoting awareness on District  council loans targeting youth, women and people with disabilities.

 In seeing the success of this league, YPM thought it is good to start this competition to bring positive development in the Mlalo Division where participating teams are from Hemtoye wards, Kilole, Kwekanga,Malindi and Malibwi. Speaking to the people who gathered to witness the opening, YPM Program Manager Mr. Peter Jally said “This competition is to bring people together to solve the various challenges facing their community, including economic and social challenges such as opposing evil actions that endanger peace in society without forgetting Gender Based Violence and opposing early marriage and Early pregnancies.”. The official guest who was the Village Chairperson of Msale Hon. Amdi Abeid is pleased with the arrival of the   YPM for bringing the competition by saying that “It is a privileged opportunity for them and they promise to make good use of the opportunity to help the youth and the community to bring personal development and the development of the Nation as a whole in sports”.

 However, the Environment and Sports Development Officer Mr. Francis Kamote encouraged the young people participating in the competition to use the opportunity they had gotten to develop their talents because sports create jobs. He also stressed the care of the environment because it is a cross-cutting issue by saying “I should ask my brothers and sisters to take care of the environment while we raise and develop talents and create an environment for people to be employed and self-employed through sports, we must remember and stand firm in the care of the environment because this issue is sensitive and cross-cutting. Environmental Protection is an issue that cannot be avoided. Life is environment and environment is life. We thank the almighty God who has enabled us to manage and achieve this matter”

The following are some photos in various events at the opening of the “Stop Poverty Cup” league. Please continue to visit our website by clicking on the link www.youthpeacemakers.or.tz for more information.