Blue Economy Seminar

Semina ya uchumi wa bluu.

Leo vijana wa YPM pamoja na vijana wa mradi wa change wamepata nafasi ya kushiriki semina ya uchumi wa bluu na kujifunza kuhusu ufugaji wa samaki na fursa zilizopo kwenye ufugaji wa samaki nyumbani kwa kijana mjasiriamali ambae pia ni kijana wa kujitolea katika ofisi za YPM. Kijana Yasini Juma ameanzisha bwawa la samaki ambapo anafuga samaki aina ya sato.

Yasini aliwaeleza kuwa wazo la biashara ndio kitu kikubwa pamoja na kulitumikia wazo hilo ili kuleta matokeo chanya. Alizidi kusisitiza kwamba vijana wanapaswa kujiamini na kutilia maanani kile wanacho kifanya ili waweze kufanikiwa.

Blue economy seminar.

Today YPM youth as well as the youth of the change project have had the opportunity to hold a blue economy seminar to learn about fishing and the opportunities in the aquaculture industry, at home of a young entrepreneur who is also a volunteer in YPM offices. Yasini Juma has set up a fish pond where he raises sato fish. Yasini has explained to them that the idea of a business is a big thing as well as serving this idea to bring about positive results.

He further emphasized that young people should be confident and considerate of what they are doing in order to be successful.