
Lushoto, Tanzania – Mkurugenzi wa Y Global, Kristin Bjørå, ametembelea ofisi za Youth Peacemakers Tanzania (YPM) kama sehemu ya ziara yake ya ukaguzi wa utendaji wa shughuli zinazotekelezwa chini ya Y Global. Ziara hii inalenga kutathmini maendeleo ya miradi, changamoto zinazokabili utekelezaji wake, na kujadili mbinu bora za kuimarisha ushirikiano kati ya Y Global na YPM.
Wakati wa ziara hiyo, Kristin Bjørå alikutana na viongozi wa YPM, wakiwemo Mkurugenzi Mwanzilishi wa YPM, Mchungaji Godfrey Tahona Walalaze, pamoja na timu ya wafanyakazi wa YPM. Majadiliano yalihusu maendeleo ya miradi inayoendeshwa na YPM, ikiwemo programu za VICOBA, michezo kwa maendeleo, na utetezi wa haki za vijana.

Aidha, Kristin alitembelea moja ya Peace Club katika Shule ya Sekondari Ngulwi, ambako aliweza kujionea jinsi wanafunzi wanavyoshiriki kikamilifu katika uoteshaji wa kisasa wa miche ya miti ya parachichi. Ujuzi huu umetolewa na wataalamu wa YPM ili kuwapa wanafunzi maarifa ya kilimo endelevu na uhifadhi wa mazingira. Ziara hii ilimpa fursa ya kushuhudia namna vijana wanavyotekeleza kwa vitendo mafunzo wanayopata kupitia programu za YPM.
“Tunajivunia kuona jinsi YPM inavyoendelea kuboresha maisha ya vijana kupitia miradi endelevu. Ushirikiano wetu na YPM una mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa vijana wanapata fursa za maendeleo na uongozi,” alisema Bjørå.

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa mazungumzo kuhusu mbinu za kuimarisha ushirikiano, hususan katika kuboresha programu za maendeleo ya vijana na uimarishaji wa uwezo wa ndani wa YPM
Y GLOBAL DIRECTOR KRISTIN BJØRA VISITS YPM OFFICES AND NGULWI PEACE CLUB
Lushoto, Tanzania – Y Global Director Kristin Bjørå visited the offices of Youth Peacemakers Tanzania (YPM) as part of her official visit to assess the performance of projects under Y Global. The visit aimed to evaluate project progress, identify challenges, and discuss best practices for strengthening collaboration between Y Global and YPM.

During her visit, Kristin Bjørå met with YPM leadership, including the Founding Director, Mchungaji Godfrey Tahona Walalaze, and the YPM staff team. The discussions focused on the progress of YPM-led initiatives, such as VICOBA programs, sports for development, and youth advocacy efforts.
Additionally, Kristin visited one of the Peace Clubs at Ngulwi Secondary School, where she observed students actively participating in modern avocado seedling cultivation. This knowledge has been imparted by YPM experts to equip students with sustainable agriculture skills and environmental conservation practices. The visit provided an opportunity for her to witness firsthand how young people are applying the training they receive from YPM programs.

“We are proud to see how YPM continues to improve the lives of young people through sustainable projects. Our partnership with YPM plays a vital role in ensuring that young people have access to opportunities for development and leadership,” said Bjørå.
The visit concluded with discussions on strengthening collaboration, particularly in enhancing youth development programs and building YPM’s internal capacity.