
Leo tarehe 22/03/2025 YPM kwa Kushirikiana na CEFA wamefanikiwa kuzindua rasmi mradi wa “uwezeshaji wa vijana na wanawake katika kujenga amani endelevu” mradi unaofanyika katika mkakati wa kutekeleza agenda ya Kujenga amani, katika Wilaya ya Mkinga kata ya Duga.

Uzinduzi huu umehudhuriwa na wadau wa maendeleo Ishirini na Tatu (23) kutoka kata Sita za mkinga ambazo ni Duga, Maramba, Kasera,Kwale, Moa pamoja na Mayomboni, kata ambazo mradi huu ndio utatekelezwa.
Mh. Hilda Muro msaidizi wa Afisa Maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga amezindua rasmi utekelezaji wa mradi huu na kuomba wadau wa maendeleo kutoa ushirikiano katika kufanikisha mradi huu.

Aidha YPM wanatarajia kutekeleza mradi huu kwa muda wa mwaka mmoja na matarajio makubwa ni kuona jamii ya Wilaya ya Mkinga inafanikiwa na kupiga hatua katika harakati za kupinga na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia, umasikini na kupigania amani ya jamii na nchi kwa ujumla.