Youth Peacemakers Tanzania (YPM) kwa kushirikiana na Tai Impact wameendesha programu maalum ya utoaji elimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia mfumo wa vikaragosi chapa tatu (3D Animation). Programu hii imelenga wanafunzi wa shule za sekondari ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uelewa wa vijana juu ya changamoto za mazingira na jinsi ya kuzitatua.

Shule zilizonufaika na mpango huu ni:
- Mlongwema Secondary
- Ngulwi Secondary
- Lushoto Secondary
- Shambalai Secondary
Kupitia teknolojia ya 3D Animation, wanafunzi wamepata fursa ya kujifunza kwa njia shirikishi na ya kuvutia, jambo lililosaidia kuboresha uelewa wao juu ya athari za mabadiliko ya tabianchi na hatua wanazoweza kuchukua ili kulinda mazingira.

YPM na Tai Impact wanaendelea kujizatiti katika kuwawezesha vijana kuwa mawakala wa mabadiliko chanya kwa kutumia mbinu za kisasa na zenye mvuto katika utoaji wa elimu.
#ClimateChange #YPM #TaiImpact #3DAnimation #VijanaNaMazingira

YPM and Tai Impact Provide Climate Change Education Through 3D Animation
Youth Peacemakers Tanzania (YPM), in collaboration with Tai Impact, has launched a unique program to provide climate change education using 3D animation. This initiative aims to raise awareness among students about the challenges of climate change and how they can contribute to addressing these issues.
The schools involved in this program include:
- Mlongwema Secondary
- Ngulwi Secondary
- Lushoto Secondary
- Shambalai Secondary

Through 3D animation technology, students have had the opportunity to engage with interactive and captivating content, which has enhanced their understanding of the impact of climate change and the steps they can take to protect the environment.
YPM and Tai Impact continue to empower youth to become agents of positive change by utilizing modern and engaging methods of education.
#ClimateChange #YPM #TaiImpact #3DAnimation #YouthAndEnvironment