YPM kwa Kushirikiana na CEFA waendelea Kutekeleza Mradi wa Kujenga Amani kwa Vijana na Wanawake

Youth Peacemakers Tanzania (YPM) kwa kushirikiana na CEFA inaendelea kutekeleza mradi wake wa kujenga amani, wenye lengo la kuwawezesha vijana na wanawake katika kuleta amani endelevu katika jamii.

Hivi karibuni, YPM kwa kushirikiana na CEFA imefanya mafunzo ya utambuzi na utatuzi wa migogoro katika shule sita zilizopo Wilaya ya Mkinga. Shule zilizoshiriki ni Zingibari Sekondari, Duga Sekondari, Manza Sekondari, Mkinga Leo Sekondari, Kwale Sekondari pamoja na Kasera Shule ya Msingi.

Lengo la mafunzo haya ni kuwapatia vijana elimu na ujuzi muhimu wa utatuzi wa migogoro, ili wawe mabalozi wa amani katika jamii zao. Kwa kuwafikia wanafunzi wakiwa bado katika hatua ya awali ya maisha yao, YPM na CEFA wanaamini kuwa wanaweka msingi imara wa kizazi kijacho kitakachothamini mazungumzo, kuelewana na njia zisizo za vurugu katika kutatua migogoro.

Hamu na ushiriki mkubwa uliodhihirishwa na wanafunzi vinaonyesha umuhimu na uhitaji wa mipango kama hii. YPM kwa kushirikiana na CEFA itaendelea kujitoa kuendeleza juhudi hizi na kuwekeza kwa vijana viongozi watakaosababisha mabadiliko chanya katika jamii.

Pamoja, tunajenga utamaduni wa amani, kiongozi mmoja kijana kwa wakati.

YPM in Collaboration with CEFA Continues to Implement Peacebuilding Project Empowering Youth and Women

Youth Peacemakers Tanzania (YPM), in collaboration with CEFA, is continuing to implement its peacebuilding project aimed at empowering young people and women to promote sustainable peace in communities.

Recently, YPM and CEFA conducted conflict identification and resolution training sessions in six schools across Mkinga District. The schools involved included Zingibari Secondary School, Duga Secondary School, Manza Secondary School, Mkinga Leo Secondary School, Kwale Secondary School, and Kasera Primary School.

The objective of these trainings is to equip young people with essential knowledge and skills in conflict resolution, enabling them to become effective peace ambassadors within their communities. By reaching students at an early stage, YPM and CEFA believe they can nurture a new generation that embraces dialogue, understanding, and non-violent approaches to conflict.

The enthusiasm and active participation from students demonstrated the importance and relevance of such initiatives. YPM, in collaboration with CEFA, remains committed to expanding these efforts and continuing to invest in young leaders who will drive positive change in their societies.

Together, we are building a culture of peace, one young leader at a time.