Siku ya Mazingira Duniani
Tarehe 5 ya mwezi wa 6 kila mwaka dunia husherehekea siku ya Mazingira Duniani, siku hii ilianzishwa rasmi na Umoja wa Mataifa mwaka 1972 ikiwa na kusudi kubwa la kueleza changamoto mbalimbali zinazokuba mazinira yetu lakini pia kusaidia kuelimisha jamii juu ya mazingira,changamoto zinzokumba mazingira na njia gani zitumike ili kutunza mazingira.Kwa mwaka huu Siku ya mazingira duniani imeazimishwa nchini Pakistani,kitaifa imeazimishwa Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma halikadhirika kiwilaya imefanyika Kata ya Lushoto katika viwanja vya Nyerere Squire.Sikuu hii imebeba kauli mbiu inayosema “KUOKOA MFUMO WA IKOLOGIA” .Katika siku hii muhimu YPM imeshiriki kutuza mazingira kwa kugawa miti na kupanda miti zaidi ya mia tatu(300) katika vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha vya kata ya Ngulwi.Meneja miradi Bwan. Peter Jally akiambatana na Afisa Mazingira na Utetezi Bi.Lidya Mshemu pamoja na wafanya kazi wengine wa YPM wamehamasisha vikundi hivyo juu ya utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti lakini pia, kwakutumia nishati mbadala. Watumishi hao wa YPM walivieleza vikundi hivyo madhara yanayotokea kotokana utonzaji mbovu ma mazingira kama mabadiliko ya hali ya hewa yaliopelekea mvua nyingi kunyesha na kuharibu mazao pamoja na miundo mbinu kwa mwaka 2020.Baada ya hapo zoezi la upandaji miti liliendelea kwenye mashamba yao ambapo wanavikundi hao walielekezwa vipimo sahihi na naamna ya kupanda miti hiyo.
The World Environmental Day
On the 5th of June every year the world celebrates World Environment Day, this day was officially established by the United Nations in 1972 with the aim of highlighting the various challenges facing our environment but also helping to educate society about the environment. This year World Environment Day has been celebrated in Pakistan, national has been celebrated at the country’s Capital City in Dodoma and District level was celebrated at Lushoto ward on the Nyerere squire ground. On this important day, YPM has been involved in protecting the environment by donating trees and planting more than three hundred (300) trees to the Community Microfinance Groups (CMGs)of Ngulwi Ward in Lushoto District. The Program Manager Mr. Peter Jally accompanied by Environment and Advocacy Officer Ms. Lidya Mshemu along with other YPM staff members have encouraged the groups on environmental protection by planting trees but also by using renewable energy The YPM staff briefed the groups on the effects of poor weather and climate change, which led to heavy rains and crop failures as well as infrastructure in 2020. After that, tree planting continued on their farms where the group members were directed on the accurate measurements and on how to plant those trees better.