Mh. Sekiboko: Wanawake tumieni teknolojia kujiendeleza
Mh. Husna Sekiboko, Mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa Tanga, ambaye ni mgeni rasmi, ameambatana na mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh. Ekalisti Lazaro pamoja na wanawake kutoka taasisi za serikali na zisizo za kiserikali kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Lushoto kufanya maadhimisho ya siku ya Wanawake Kimataifa yaliyoadhimishwa kiwilaya katika Kijiji cha Lunguza kata ya Lunguza tarehe 8 mwezi machi 2023, wakiongozwa na kaulimbiu “Uvumbuzi na maendeleo ya kiteknolojia kwa usawa wa kijinsia”.
Mh. Sekiboko amesema wanawake wanapaswa kutumia teknolojia ya mawasiliano kujiendeleza kibiashara na kuwafundisha wanawake wengine mbinu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi kwa kutumia simu za mikononi. Pia amewaasa wazazi kuwaelekeza watoto wao matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kujiendeleza kielimu kuliko kutumia muda mwingi katika kuperuzi tovuti na kurasa zisizo na maadili.
“Wanaume wanapaswa kushirikiana na wanawake katika kulea familia kwa upendo na sio kuwaachia wanawake wenyewe’, amesema Mh. Sekiboko. Halikadhalika amepinga vikali uwepo wa mila potofu ambazo humkandamiza mwanamke kama vile kurithi mke wa marehemu kwani ni mila inayohatarisha usalama wa afya ya mwanamke anayerithiwa.
Upande wa kupinga ukatili wa kijinsia Mh. Sekiboko amesema wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto wao michezo yenye staha, michezo ambayo haitawafanya watu wengine wawatamani watoto kutokana na maumbile, hivyo si vyema mzazi kumruhusu mtoto kunengua mbele za watu ili kumkinga na unyanyasaji wa kijinsia.
YPM Tanzania imeazimisha siku hii kwa kuanza na shughuli mbalimbali za usafi katika eneo la ofisi ya YPM siku ya jumamosi tarehe 4 machi, kisha kufuatia na ugawaji wa taulo za kike katika shule ya Prince Claus, ambako waliambatana na wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, wafanyakazi wa ustawi wa jamii pamoja na redio Utume.
Women should use technology for their own development, Ed. Sekiboko
Hon. Husna Sekiboko, Member of Parliament for CCM special seats in Tanga region, who is an official guest, has accompanied the head of Lushoto District Hon. Ekalisti Lazaro together with women from government and non-government organisation from various parts of Lushoto district to celebrate the International Women’s Day celebrated in the district in Lunguza Village, Lunguza ward on March 8, 2023, and the slogan was “innovation and technology for gender equality”
Hon. Sekiboko said that women should use communication technology to develop themselves commercially and teach other women various ways to get help themselves economically by using mobile phones. She also urged parents to direct their children to the correct use of social networks to help them develop themselves educationally instead of spending a lot of time browsing immoral websites and pages.
“Men should cooperate with women in raising a family with love and not leave it to women themselves”, said Hon. Sekiboko Furthermore, she strongly opposed the existence of stereotypes that oppress women, such as inheriting the wife of the deceased, as it is a tradition that endangers the health of the inherited woman.
On sexual violence issues Hon. Sekiboko said that parents should teach their children decent games, games that will not make other people want to exploit children, so it is not good for a parent to allow a child to play in front of people to protect him from sexual abuse.
YPM Tanzania has commemorated this day by starting with various cleaning activities in the area of the YPM office on Saturday 4 March, then following with the distribution of female towels (pads) at Prince Claus Secondary School, where they were joined by the staff of the Lushoto District Council, social welfare workers as well as Utume radio workers.