GBV training

Norec exchange participant hosted a two-day GBV training with volunteers from YPM who were passionate about learning and eager to join the community to raise awareness!

SIGs Monitoring and Evaluation

Ufuatiliaji wa Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Kifedha .

YPM imeendela kutembelea na kutatua changamoto mbambali ambazo Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Kifedha vinakumbaza nazo hasa katika swala zima la uwendeshaji wa vikundi hivi. awamu hii YPM imepata nafasi ya kutembelea vikundi vya Mbumbuli Msongolo na Funta.

Monitoring of Microfinance Social Groups.

YPM has continued to visit and solve the various challenges that Community Microfinance Groups are facing, especially in the whole issue of the operation of these groups. In this phase YPM has had the opportunity to visit the groups of Bumbuli Msongolo and Funta.

Young Facilitator Training

Mafunzo ya wawezeshaji Vijana

Tarehe 18 na 19 Desemba 2023 YPM iliendesha mafunzo ya wawezeshaji vijana wa Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Fedha kutoka maeneo ya Malibwi, Bumbuli, Ngulwi, Korogwe , Makanya na Magamba. Kama taasisi inayojihusisha na maendeleo ya vijana ilikuomboa jamii, YPM imeweka mkazo katika kuwawezesha vijana hawa ili waweze kuwawezesha wengine katika uwanzishaji na usimamizi wa vikundi hivi, ili sheria, kanuni na taratibu zilizoweka na Serikali ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania zifuate ilikuleta maendeleo endelevu katika jamii.

Young SIGs Facilitators training

On the 18th and 19th of December 2023 YPM conducted the training of young facilitators of the Community Microfinance Groups (CMGs) from the areas of Malibwi, Bumbuli, Ngulwi, Korogwe, Makanya and Magamba. As an organisation that is involved in the development of young people in the community, YPM has focused on empowering these young people so that they can empower others in the establishment and management of these groups, so that the laws, regulations and procedures set by the Government of the United Republic of Tanzania are followed to bring sustainable development in the community.

Youth Change Summit (YCS)2023

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Khamis amewakumbusha vijana wenye uelewa kuhusu mazingira kutoa elimu hiyo kwa wananchi wa vijijini wasio na uelewa juu ya athari za uharibifu wa mazingira  ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema hayo katika ufunguzi wa Kongamano la vijana la Youth Change Summit linalojadili mada mbalimbali za mabadiliko ya tabia nchi lililo fanyika  kwa siku mbili wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo amesema ni wakati wa vijana wasomi kuipeleka elimu hiyo maeneo ambayo hayafikiki kirahisi ili kujenga uelewa juu ya athari na madhara yatokanayo na uharibifu wa mazingira.

Participants of YCS 2023

Katika hotuba yake pia Mh.Khamis amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa majiko banifu ambayo yanasaidia kupunguza au kuondosha kabisa vitendo vya ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa sambamba na kuhamasisha matumizi ya mkaa mbadala.

Katika hatua nyingine amebainisha Serikali inaendelea na utaratibu wa kupunguza Kodi Katika nishati mbadala ili wananchi waweze kustahimili kwa kila kaya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya Youth PeaceMakeres Tanzania Mch. Godfrey Tahona Walalaze amesema wamelenga kufanya Kongamano hili la Mazingira kwa kulenga Mabadiliko ya tabia Nchi kwakuwa linaathiri maisha ya binadamu kwa ujumla  na wakiamini vijana wanauwezo mzuri wa kubuni njia bora za kukabiliana na chanzo na athari ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa maisha ya Sasa na baadae.

Youth Change Summit (YCS) 2023

Kongamano la vijana la Youth Change Summit linalofanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro linalohusu Mabadiliko ya Tabia

Nchi,Kongamano hili limefunguliwa hii na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis

Washiriki wa YCS 2023

Youth Change Summit

Youth Change Summit

Youth Change Summit 2023, is centred around the theme “Climate Change: Adapting to Climate Change and Enhancing Resilience.” Which will be held in Kuringe Hall Moshi from November 16-17,2023.

Agenda:

The Youth Change Summit will encompass a series of keynote speeches, panel discussions, workshops, and interactive activities designed to empower youth in the following key areas:

  • Embracing Climate Innovation: Pioneering Solutions for a Sustainable Future.
  • Breaking Barriers, Building Resilience: Advancing Gender Equality in Climate Action.
  • Cultivating -a sustainable Workforce: Uniting for green jobs and -a greener Future

04.Elevating Voices, Driving Change: Empowering climate advocacy for a sustainable Tomorrow.

 Youth Change Summit 2023, umejikita kwenye mada “Mabadiliko ya Tabia ya nchi: Kukabiliana mabadiliko ya tabia ya nchi na kuimarisha Ustahimilivu.” Ambao utafanyika katika ukumbi wa Kuringe Moshi kuanzia Novemba 16-17,2023.

Ajenda:

Mkutano wa Youth change summit utajumuisha mfululizo wa hotuba kuu, mijadala ya jopo, warsha, na shughuli shirikishi zilizoundwa ili kuwawezesha vijana katika maeneo muhimu yafuatayo:

01. Kukumbatia ubunifu wa kushulikia changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi: Suluhu za uanzilishi kwa mustakabali endelevu.

02. Kuvunja Vikwazo, Kujenga Ustahimilivu: Kuendeleza Usawa wa Kijinsia katika kuchukua hatua juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi.

03. Kukuza nguvukazi endelevu: Kuungana kwa ajili ya kazi za kijani.

04.Kupaza sauti, kuendesha mabadiliko: Kuwezesha utetezi wa hali ya hewa kwa kesho endelevu.

Youth Initiative

”Wema kidogo wa leo huifanya kesho kuwa bora”

 Haya ni maneno yaliokuwa yakipamba katika vipeperushi vya mtandaoni vilivyo andaliwa na wanachama wa peace club wa shule ya Secondari Mlongwema. Hii ni kutoka na jitihada walizo anzisha vijana hawa katika kuendeleza kampeni ya kutokomeza umaskini, mimba na ndoa za utotoni katika maeneo ya Mlola na Ngwelo wilayani Lushoto.

Vijana hawa walikuwa wanachama wa peace club ilioyokua inayosimamiwa na YPM, ambapo YPM Ilitoa mafunzo mbali mbali ya utunzaji wa mazingira, usawa wa kijinsia, kuhamasisha elimu bora pamoja na afya bora haya yote ya kiwa ni malengo endelevu ya dunia, lengo no.13,5,4 na 3. YPM inayofurha kubwa kuona vijana hawa ambao kwa sasa wapo vyuo vikuu nchini, kwamba wametambua nafasi walioyonayo nakurudi kuwasaidia wadogo zao wenye uhutaji wa vifaa vya shule na usafi binafsi ambapo vijana hawa walitoa mashati ya shule, sabuni za miche na unga, madaftrari katoni mbili, taulo za kike, kalamu na vifaa vingine vya shule kwa wanafunzi.

YPM pamoja na washirika wake kutoka Valdres Norway waliweza kuunga mkono jitihada hizo kwa ushiriki wa pamoja katika shule ya Sekondari Mlongwema. YPM imepongeza na kuhamasisha vijana wetu wa peace club kutumia elimu wanayopata ilikusaidia na kuikomboa jamii kutoka kwenye dimbwi la umasikini.

”A little kindness today makes tomorrow better”

These are the words that were used in the online flyers prepared by the peace club members of Mlongwema Secondary School. This is from the efforts initiated by these young people in continuing the campaign to eradicate poverty, early marriage and early pregnancy in the areas of Mlola and Ngwelo in Lushoto district. These young people were members of the peace club which is being facilitated by YPM, where YPM provided various trainings on Climate Action, Gender Equality, Quality Education and Good Health and Well-Being amongst other, for which are sustainable development goals (SDG), goal no. 13,5, 4 and 3.

 YPM is very happy to see these young people who are currently in universities in the country, that they have realized the opportunity they have and come back to help their younger ones who are in need of school supplies and personal hygiene where these young people donated school shirts, bar and powder soaps, notebooks in two cartons, sanitary towels, pens and other school supplies for students.

YPM together with its partners from Valdres Norway were able to support those efforts with joint participation at Mlongwema Secondary School. YPM also has congratulated them and encourages young people from peace club to use the education they get to help and free the community from the braking the chains of poverty.

NOREC

We have had the chance to say goodbye to our colleagues who we were together for a period of one-year as NOREC participants 2022/2023 (Norwegian Exchange Cooperation). We acknowledge the work contribution from Norwegian participant M/S Cecilia Grevstad and from Ethiopia Dr. Yordanos Alem Hagos. Today marks the end of their stay here at YPM, we thank them very much for their presence, we have managed to learn a lot from they, and they have become a great help to the organisation. YPM is very proud of them.

Tumepata nafasi ya kuwaaga watumishi wenzetu tuliokua nao katika program NOREC (Norwegian Exchange Cooperation) ya mwaka moja kutoka nchi ya Norway M/S Cecilia Grevstad and kutoka Ethiopia Dkt Yordanos Alem Hagos. Leo ikiwa siku ya mwisho kwao kuwepo pamoja nasi tunawashukuru sana kwa ajili ya uwepo wao tumefanikiwa kujifunza mengi wamekua msaada mkubwa sana tunawatakia safari njema kila mmoja anaporudi nchini kwake na tunafurahi kuongeza wanafamilia YPM.

International Youth Day

International Youth Day

 is a wonderful opportunity to engage and empower young people, fostering their involvement in creating a more sustainable future through education, advocacy, and meaningful initiatives? It is a chance to inspire them to take action, contribute to positive change, and address pressing global challenges like climate change, social justice, and economic inequality. By providing platforms, resources, and support, we can help shape a generation that actively participates in building a better world.

On this day of 12 August YPM gathered young people to celebrate International youth day. Various topics were discussed and the event was closed by rewarding individuals who represent others on the effort to fight against poverty and injustice.

Siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani

Inatupa fursa ya kuwashirikisha na kuwawezesha vijana, kukuza ushiriki wao katika kuunda zaidi mustakabali endelevu kupitia elimu, utetezi, na mipango ya kibunifu. Ni nafasi ya kuwatia moyo kuchukua hatua, kuchangia mabadiliko chanya, na kushughulikia changamoto kubwa za kimataifa kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, haki za kijamii, na ukosefu wa usawa wa kiuchumi. Kwa kutoa majukwaa, rasilimali, na kuunga mkono, tunaweza kusaidia kuunda kizazi ambacho kinashiriki kikamilifu katika kujenga ulimwengu bora. Siku hii ya tarehe 12 Agosti YPM ilikusanya vijana kusherehekea siku ya ndani ya vijana. Mada mbalimbali zilijadiliwa na hafla hiyo ilifungwa na kuwazawadia watu wengine katika juhudi za kupambana na umaskini na dhuluma.