Entrepreneurship training

Leo tumekua na semina nzuri ya ujasiliamali iliongozwa na Program Manager Peter Jally.

Today we had an interesting training of business Entrepreneurship led by Program manager Peter Jally.

SDGs training

Semina ya Maendeleo Endelevu ya dunia.

YPM imeendesha semina iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya YPM hapa Lushoto. Semina hiyo ililenga kusaidia vijana kuongeza uelewa juu ya Maendeleo Endelevu ya Dunia. Vijana Arobaini (40) kutoka klub za amani za shule za sekondari za Shambalai na Ubiri walishiriki mafunzo hayo. Mafunzo haya yamelenga kuwajengea vijana  uelewa zaidi juu ya Malengo endelevu ya dunia hususani zaidi ni lengo namba 13 ambalo linahusu maswala mazima ya utunzaji wa mazingira somo ambalo lilitolewa na kijana wa kujitolea ndugu.Tahona Godfrey. Somo la pili lilitolewa na Dkt Glory Kimario ambapo alifafanua juu ya lengo namba 5 usawa wa kijinsia na kusisitiza ni kwa jinsi gani vijana wa kike na wa kiume wanaweza kushiriki pamoja katika kuleta maendeleo. AKizungumza na vijana hao Meneja Miradi wa YPM Bwana Peter Jally aliwaasa vijana hao kushiriki kikamilifu katika kutekeleza malengo hayo ya dunia. Aidha, Mkurugenzi wa Taasisi ya YPM Mch. Godfrey Walalaze alipata wasaa wa Kuzungumza na vijana na kuwaeleza juu ya umuhimu  wakunyambua kila lengo vizuri na kujua malengo madogomadogo yalioko kwenye kila lengo ili kurahisisha utekelezaji katika vikundi vyao vya amani mashuleni lakini pia hata katika jamii zao.

YPM inapenda kupongeza shule zote zilizoshiriki, walimu na washiriki wote kwa ujumla katika jitihada hizi endelevu za kujenga uelewa na kurahisisha utekelezaji wa Malengo Endelevu ili kuhakikisha hakuna anae achwa nyuma.

Sustainable Development Goals Seminar.

YPM conducted a seminar held at the YPM office grounds here in Lushoto. The seminar aimed at helping young people raise awareness about Sustainable Development Goals (SDGs). Forty (40) young people from Shambalai and Ubiri peace schools’ clubs participated in the training. This training aims to build young people’s understanding of the Sustainable Development Goals and in particular is goal number 13 which deals with the whole issue of environmental protection a session facilitated by a young volunteer Tahona Godfrey. The second session was delivered by Dr. Glory Kimario where she elaborated on goal number 5 gender equality and emphasized on how young women and men can participate together in bringing about development. Speaking to the youth, YPM Program Manager Mr. Peter Jally urged the youth to actively participate in the pursuit of these global goals. In addition, YPM Institute Director Rev. Godfrey Walalaze had the opportunity to talk to young people and explain to them the importance of tackling each goal well and knowing the sub-goals in each goal to facilitate implementation in their peace groups in schools but also in their communities.

YPM would like to appreciate and thanks all schools, teachers and all participants in this ongoing efforts to build awareness and facilitate the implementation of the Sustainable Development Goals to ensure that no one is left behind.

Blue Economy Seminar

Semina ya uchumi wa bluu.

Leo vijana wa YPM pamoja na vijana wa mradi wa change wamepata nafasi ya kushiriki semina ya uchumi wa bluu na kujifunza kuhusu ufugaji wa samaki na fursa zilizopo kwenye ufugaji wa samaki nyumbani kwa kijana mjasiriamali ambae pia ni kijana wa kujitolea katika ofisi za YPM. Kijana Yasini Juma ameanzisha bwawa la samaki ambapo anafuga samaki aina ya sato.

Yasini aliwaeleza kuwa wazo la biashara ndio kitu kikubwa pamoja na kulitumikia wazo hilo ili kuleta matokeo chanya. Alizidi kusisitiza kwamba vijana wanapaswa kujiamini na kutilia maanani kile wanacho kifanya ili waweze kufanikiwa.

Blue economy seminar.

Today YPM youth as well as the youth of the change project have had the opportunity to hold a blue economy seminar to learn about fishing and the opportunities in the aquaculture industry, at home of a young entrepreneur who is also a volunteer in YPM offices. Yasini Juma has set up a fish pond where he raises sato fish. Yasini has explained to them that the idea of a business is a big thing as well as serving this idea to bring about positive results.

He further emphasized that young people should be confident and considerate of what they are doing in order to be successful.

Health Education Training

Health Education Training

Washiriki wa Mradi wa Change wakiwa na vijana wengine wakati wa mafunzo ya Elimu ya Afya na Makuzi ya vijana yaliongozwa na Mtaalamu wa Afya kutoka katika Hospitali ya Wilaya Hai (Boma) Dr. Glory Kimario ambae pia ni kijana wa kujitolea katika ofisi za Youth Peacemakers hapa Lushoto. Dhumuni la mafunzo hayo nikuwawezesha vijana kuongeza uwelewa juu ya afya zao na kujua jinsi gani wanaweza kukabiliana na changamoto za kifya ili pia waweze kuwasaidia wengine katika jamii zao kutatua changamoto hizo.

Change participants during the training

Taifa imara linategemea vijana hivyo imara kwa vijana ndio nguvu ya maendeleo.

Mafunzo ya Elimu ya Afya.

Participants during the training

Change Project Participants with other young people during the Health Education and Youth Growth Development training led by a Health Specialist from Hai District Hospital (Boma) Dr. Glory Kimario who is also a young volunteer at the Youth Peacemakers offices here in Lushoto. The purpose of the training is to enable young people to raise awareness about their health and to know how to cope with health challenges so that they can also help others in their community to solve these. challenges.

Dr. Glory Kimario facilitating

The power of a nation depends on the power of the young people.

Welcome Our Partners from Norway

Welcoming our partners from Y-Global to YPM.

We are very pleased to welcome you to the YPM and we hope you will have a nice stay here in Lushoto.

Karibuni wageni wetu kutoka Norway.

Rev. Godfrey Walalaze at the middle speaking to the guests from Norway

Tunafurahi sana kuwakaribisha Lushoto na ni matumaini yetu mtafurahia.

Debate

This Friday Shambalai Secondary School had a Debate with Mombo Secondary School on the topic ” Science and Techonology have brought more harm than good in third world countries”

We are happy that young people had managed to argue and share their thoughts about the topic.

International Celebration of Women’s Day

Maazimisho ya siku ya wanawake duniani.

Kila tarehe 8 ya mwezi Machi dunia inasheherekea siku ya wanawake duniani. Katika ngazi ya Wilaya YPM imeungana na maasifa wa serikali wakiongozwa na mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa Wilaya Lushoto Mheshimiwa Karisti Lazaro, Mkurgenzi mtendanji mheshimiwa Ikupa Mwaisyoge pamoja na maafisa wengine. Maadhimisho hayo yalikua na kaulimbiu isemayo ”Usawa wa kijinsia wa leo,kesho na endelevu”.Sio hivyo tu bali wanachi na wanafunzi walijitokeza kwa wingi kusheherekea siku hiyo.

World Women’s Day celebrations.

Every March 8th the world celebrates International Women’s Day. At the district level YPM is joined by government officials led by the official guest who is Lushoto District Commissioner Hon. Karisti Lazaro, Executive Director Hon. Ikupa Mwaisyoge and other officials. The theme of commemoration was “Gender equality today, tomorrow and sustainability”. Not only that but citizens and students turned out in large numbers to celebrate the day.

Young Person who managed to save the World

Young Person who managed to save the world.

It is from YPM Peace Club to the Environment Champion.

Meet Leonard Antony Msumari who completed his O-level studies in 2021 at Prince Claus Secondary School in Lushoto district. Leonard is 19 years old and lives with his parents in the village of Irente which is about two and a half miles from where he lives. When he started his studies in 2018 he joined the YPM Peace club which has been established by the YPM Tanzania Organisation for the purpose of mobilizing young people on environmental stewardship. While working with the YPM Peace club, Mr. Antony expressed admiration for the way the club grew up caring for the environment by organizing tree nurseries and planting trees. Leonard not only actively participated in the club activities and showed his ability and high motivation in the club, but also took the distributed trees and planted them in their fields. However, Mr. Antony became more interested in setting up a nursery at his home place. Speaking to YPM staff, Mr. Antony said that he has so far sold 36000 trees to the community members and planted a total of 1500 trees from last year to now. YPM staff are pleased to see young people actively involved in liberating the world and find the solution for tackling the issue of climate change. Congratulations to Mr. Leonard Antony on this milestone and we are behind him to support him in this movement. Our call to the youth is to support the efforts of rescuing the world from the challenges which are being brought by climate change.

Kijana aliefanikiwa kuikoa dunia.

Ni kutoka YPM klabu ya Amani mpaka mpigania haki za mazingira.

Kutana na Leonarld Antony Msumari ambae ni  ni mwanafunzi aliehitimu masomo yake ya kidato cha nne mwaka 2021 katika  Shule ya Secondari Prince Claus Hapa wilayani Lushoto. Leonard ana umri wa mika 19 na anaishi na wazazi wake katika kijiji cha Irente ambapo ni kilometa takribani mbili na nusu kutoka nyumbani anapoishi. Wakati alipoaanza masomo yake mwaka 2018 alijiunga na YPM Peace club ambayo imeanzishwa na taasissi ya YPM Tanzania kwa lego la kuwahamasisha vijana juu ya utunzaji wa mazingira. Alipokua kwenye YPM Peace club ndugu Leonard alionyesha kufurahishwa na jinsi club hiyo ilivyokua inatunza mazingira kwa kuandaa vitalu vya miti na kupanda miti. Leonard alishiriki kikamilifu lakini pia hakuishia kuonyesha uwezo wake na hamasa ya juu shuleni tu, bali alichukua miti waliogaiwa nakuipanda kwenye mashamba yao. Hata hivyo ndugu Leonard alivutiwa zaidi na akaanzisha kitalu cha miti nyumbani kwao. Akizungumza na wafanyakazi wa YPM ndugu antony amesema kwamba mpaka sasa ameuza miti 36,000 na amepanda jumla ya miti 1500 toka mwaka jana hadi sasa. Uongozi wa YPM umefurahishwa sana kuona vijana wanashiriki kikamilifu katika kuiokoa dunia na mabadiliko ya hali ya hewa. Tunampongeza sana ndugu Leonard kwa hatua hii aliofikia nakwamba tupo nyuma yake kumuunga mkono katika harakati hizi.Wito wetu kwa vijana nikuwaomba kuunga jitihanda zinazofanywa na dunia ilikuiokoa kutoka kwenye janga la mabadiliko ya hali ya hewa.

Take Charge for Our Future

Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa inayosumbua dunia. Hii nikutokana na kuambatana na majanga makubwa Kama vile ukame au mafuriko ambayo huhatarisha maisha ya mwanadamu hapa duniani. Katika jitihada za kupambana na changamoto hii, Ubalozi wa uholanzi nchini Tanzania uliandaa mkutano uliokutanisha takribani vijana 100 kutoka sehemu mbalimbali katika jengo la taasisi ya Alliance Françise jini Dar es salaam kwa lengo la kuwahamasisha vijana kuchukua jukumu la kuyalinda mazingira kwa vitendo  ilikuifanya dunia kuwa sehemu salama kuishi.

Mkutano ulifunguliwa na salamu za ukaribisho kutoka kwa balozi wa Uholanzi nchini Tanzania na wazungumzaji rasmi walikua ni vijana wanaharakati wa kutetea mazingira na kila mmoja alieleza hadithi yake ambayo Ilikua na mguso wa namna yake tangu alipoanza harakati hadi aliposasa. Hadithi zao zilikua hamasa kubwa kwelikweli kiasi cha kumfanya kila kijana akiwa na ari ya kutaka kupanda miti Kama sehemu ya kuyalinda na kuyatunza mazingira.

Katika kipindi cha maswali na majibu ilibainika kuwa shauku ya kutaka kupunguza mabadiliko ya tabia ya nchi ni kubwa sana kuliko matendo yanayofanyika, hii nikutokana na kuwa na sera nzuri na elimu pia, lakini changamoto yake ni kwamba havimpi ulazima mwanamchi kulibeba jukumu la kuyalinda mazingira.

Makubaliano ni kwamba changamoto hii iendelee kuzungumzwa kukuza uelewa wa raia lakini lazima zitafutwe mbinu zitakazomlazimisha kila mmoja kutunza mazingira ama akiwa anataka au hataki kwakuwa hata katika familia unaweza kuandaa chakula kizuri kinachoweza kumfanya mtoto awe na afya tele lakini yeye akakataa kula. Hivyo lazima itafutwe mbinu alazimishwe kula ilianufaike na chakula kile. Vinginevyo mikutano ya namna hii itakosa nguvu kwanza itakuwa ikijadili tu na kuandaa mikakati mizuri lakini utekelezaji hakuna na changamoto itabaki palepale.

Kutoka Taasisi ya Vijana Waleta Amani Tanzania vijana 13 walipata nafasi ya kushiriki mkutano huo. Mbali na kukuza uelewa na hamasa kutoka kwa vijana wenzao walipata wasaa mzuri wa kutengeneza marafiki wapya kutoka taasisi mbalimbali zilizo hudhuria hivyo kuifanya familia ya Vijana Waleta Amani kutambulika na kuwa kubwa zaidi.

Climate change is a major challenge facing the world. This is due to the presence of major disasters such as droughts or floods that endanger human life on earth. In an effort to address this challenge, the Dutch Embassy in Tanzania organized a conference that brought together about 100 young people from various parts of the Alliance Françise building in Dar es Salaam with the aim of motivating young people to take responsibility for environmental protection to make the world a better place to live.

The meeting was opened with welcome greetings from the Dutch Ambassador to Tanzania and the official speakers were young activists and each told his own story which was very inspiring and have its kind of impact from the beginning to the present. Their stories very impressive that they made every young person want to plant trees as part of protecting and caring for the environment.

During the question-and-answer session it was found that the desire to reduce climate change is far greater than the actions taking place, this is due to having good policies and education as well, but the challenge is that they do not give citizens the responsibility to protect the environment.

The consensus is that this challenge should continue to be discussed to raise public awareness but strategies must be employed that will force everyone to take care of the environment whether they want it or not because even in the family you can prepare healthy food that can keep a child healthy but he or she refuses to eat. So a method must be employed to force him to eat in order to benefit from that food. Otherwise meetings of this nature will lack strength first will only discuss and devise good strategies but no implementation and challenges will remain the same.

From the YPM Tanzania 13 young people had the opportunity to participate in the conference. In addition to nurturing understanding and motivation from their peers, they also had the opportunity to make new friends from various attending Organization, thus making the YPM family big recognizable.