Stop Poverty Final

YPM imehitimisha mashindano ya Stop Poverty Cup Football League huko wilayani Mkinga mkoani Tanga. Mshindano haya yalipambwa na jumbe mbalimbali zikisomeka katika mabango na kuelezewa vizuri na Afisa michezo kwa maendeleo Bwana Francis Kamote. Moja ya jumbe ambazo zilisomeka kwenye mabango ni ujumbe wa kutokomeza ndoa za utotoni na mimba za utotoni ambapo ujumbe huu ulimgusa mgeni rasmi ambae alikua mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya Mkinga.

Akizungunza baada ya kupewa kipaza sauti aliishukuru taasisi ya YPM kwakunzaisha mpango mzuri wa kushirikiana na jamii ya watu wa Mkinga ili kutokomeza umasikini pamoja na changamoto za ndoa za utotoni na mimba za utotoni. Aidha, aliendelea kwa kukiri kwamba changamoto hii ya mimba za utotoni na ndoa za utotoni bado inaendelea kupasua vichwa vya serikali ya Mkinga na watu wenye nia njema yakutokomeza vitendo hivyo na kwamba anaunga mkono juhudi hizi ili kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya kupata elimu.

Baada ya hayo Meneja miradi wa YPM Bwana Peter Jally aliwahakikishia wananchi kwamba taasisi itaendeleza ushirikiano na jamii na serikali kuhakikisha vitendo kama hivyo vinatokomezwa.

YPM has concluded the Stop Poverty Cup Football League tournament at Mkinga district in Tanga region. The competition was adorned with various messages being read on the posters and well explained by the Sports for Development Officer Mr. Francis Kamote.

One of the messages that was read on the posters was a message on the eradication of Child Marriage and Early Pregnancy where the message touched the guest of honor who was a representative of the District Commissioner as well as the Executive Director of Mkinga District Council. Speaking after receiving the microphone, he thanked YPM for developing a good program to work with the Mkinga community to eradicate poverty as well as the challenges of Child Marriage and Early pregnancy.

In addition, he went on to acknowledge that the challenge of Early Pregnancy and Child Marriage still continues to blow the heads of the Mkinga government and people with good intention to eradicate such practices and that he supports these efforts to ensure children get their right to education. After that YPM Program Manager Mr. Peter Jally assured the public that the organisation will continue to work with the community and the government to ensure that such acts are eradicated.

SIGs follow-up and Training

Mnamo mwezi wa Tisa 09 na 10 mwaka huu YPM, iliongozwa na Meneja Miradi na Afisa  wa mpango wa  Kutokomeza Umaskini, Bwana Peter Jally, iliweza kutembelea vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za kifedha vya Handeni na Kabuku (CMGs).

Katika mpango huo, YPM inahakikisha vikundi hivi vinasonga mbele kwa kuvitembela na kutatua changamoto mbalimbali zinazokumba vikundi hivyo. Uongozi kutoka Ofisi ya Vijana wa Waleta Amani umeendesha semina ya ujasiriamali, kusajili vikundi vidogo vya huduma ndogo za kifedha, na kukumbushia kuhusu sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza  vikundi hivi. Sio hivyo tu, lakini YPM ametembelea kituo cha kompyuta cha Handeni kinachosimamiwa  na vikundi vya Handeni ili kuona  maendeleo yake.

On September 09 and 10 this year, YPM, led by Program Manager and Economic Justice Program Officer, Mr. Peter Jally, was able to visit Handeni and Kabuku Community Microfinance Groups (CMGs). In this ongoing visit, YPM ensures that, these groups move forward to reach their goals.

The officers from the Youth peacemakers Tanzania provided an entrepreneurship training, registration of the Community Microfinance Groups (CMGs), as well as reviewing the rules, regulations and procedures for running these groups. Not only that, but YPM has visited the Handeni computer center run by Handeni Community Microfinance Groups and monitoring its progress.

TIMUN 2021-Zanzibar

Youth Peace makers Tanzania has set 5 young people to participate in the Tanzania Model United Nation 2021. The aims were to provide in-depth knowledge on SDGs through sharing of ideas and views from other during the meeting, to help youth advocate for their participation in the implementation of SDGs decade of action and create a favorable and promising future for both young people and future generation.

Not only that but also, to integrate youth to the big platform where they can get exposure and grow on issues of leadership and diplomacy as they observe the rules and procedure of United Nation General assembly, to reflect on various challenges facing youth all over the word and raise voice in critical mattes not only that but also to increase knowledge and experience exchange since it connects youth from different countries in the world.

The Mkinga Stop Poverty Cup

Taasisi ya YPM imeendelea kuendesha mashindano ya Mkinga Stop Poverty Cup Football league yanayofanyika kila mwaka katika Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga. Mashindano haya yameleta manufaa makubwa sana katika jamii ya watu wa Mkinga kama alivyozungumza Diwani wa Kata ya Moa, “Naishukuru Taasisi ya Youth Peace Makers Tanzania kwakutuletea mashindano haya ambayo yamewafanya vijana kujihusisha kikamilifu katika shughuli za michezo na maendeleo na kupunguza vitendo vya wizi mtaani”.

YPM inafurahi kuona kwamba malengo ya kuanzisha mashindano haya ya mpira wa miguu yanafikiwa hususani kuwakomboa vijana kutoka katika wimbi la umasikini kwa kutumia vipaji vyao ilikujipatia kipato. Pamoja na hayo mashindao haya yalianzishwa ili kutokomeza vitendo vya kigaidi na kuwafanya vijana wajitambue na kukataa kutumiwa na watu wenye nia mbaya ya kuchafua amani.

Ikumbukwe Wilaya Mkinga ni moja ya Wilaya zilizopo mpakani na mara kadha kumekua kukiripotiwa uwepo wa makundi na watu wageni wenye nia mbaya yakutaka kuvuruga amani. Tunashukuru kwamba kupitia mashindano haya vijana wameweza kujitambua na kutambua nafasi zao katika jamii. Tunapenda kutoa pongezi kwa vikundi vya PeaceMakers vinavyotoa huduma ndogo za fedha katika jamii vya Kijiru na Karoyo (Comunity Microfinance Groups) ambavyo vimeshirikiana na kuandaa mashindano haya. Pia tunashukuru vijana wote, wazee na viongozi wa serikali walioshiriki katika mashindano haya.

YPM has continued to run the Mkinga Stop Poverty Cup Football league which is usually held annually at Mkinga District in Tanga Region. The competition has brought great benefits to the Mkinga community, as Moa ward Councilor said “I thank the Youth Peace Makers Tanzania orgaisation for bringing us this competition, this competition has made young people actively involved in sports and development activities and reduce acts of violence and street theft “.

YPM is pleased to see that the goals of establishing this football tournament are being achieved in particular to liberate young people from the chains of poverty by using their talents to generate income. However, the competition was launched to eradicate terrorism and to make young people aware of and refuse to be manipulated by people with malicious intent to disturb the peace.

It should be noted that, Mkinga District is one of the border districts and there have been several reports of groups and foreigners with malicious intent to disrupt the peace. We are grateful that through this competition young people have been able to identify themselves and realize their place in society.

We would like to congratulate the Peacemakers groups of Kijiru and Karoyo who provide financial services to the communities (Community Microfinance Groups) and had collaborated and organized this competition. We also thank all the young people, the elderly and government officials who participated in this competition.

Shambalai Sec Peace Club

Shambalai Sec School Peace Club

Leo taasisi ya YPM imepata nafasi kushiriki siku ya vijapaji Katika shule ya upili Shambalai nakujionea vipaji vya uimbaji, uigizaji, mitindo, skauti, nyimbo na maigizo kutoka katika klabu za amani shuleni hapo.

Nifuraha yetu kuona vijana wanatambua vipaji vyao na kuvitumia katika kuleta maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

The International Youth Day

                                    MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA KIMATAIFA

Siku ya vijana duniani ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1999 na kuidhinishwa mwaka 2000. Lengo la siku hii ni kuhamasisha uangalizi wa masuala ya kitamaduni na kisheria yanayowahusu vijana.Siku ya vijana duniani huadhimishwa kila mwaka. Tarehe 12 ya mwezi wa 8 imeidhinishwa kama fursa kwa serikali na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali kuwaleta vijana pamoja na kuwaongoza waweze kujadili mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa Maisha yao. Maadhimisho haya huambatana na matamasha, warsha, hafla za kitamaduni, na mikutano ambayo hufanyika ulimwenguni kote nakuhusisha maafisa wa serikali kitaifa, serikali za mitaa na mashirika ya vijana.

Taasisi ya Youth peacemakers (YPM) huadhimisha kuzaliwa kwake tarehe 12 ya mwezi wa 8 kila mwaka sambamba na maadhimisho ya siku ya vijana duniani.  Katika sherehe ya kuadhimisha siku ya vijana duniani taasisi ya Youth Peace Makers iliandaa kongamano la vijana tarehe 14.08 lenye kauli mbiu ya “UIMARISHAJI WA MIFUMO YA CHAKULA KATIKA UKUAJI WA AFYA YA AKILI NA MWILI KWA VIJANA” ikiwa ni kilele cha siku hiyo ya vijana kimataifa kwa taasisi. Kongamano hilo lililohudhuriwa na vijana kutoka shule mbalimbali za sekondari zilizopo katika wilaya ya Lushoto Kama vile Shambalai, Lushoto,Ubiri na Prince Claus. Lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha vijana kutumia vyakula vya asili katika ukuaji wa afya ya akili na mwili. Vijana hao walipata fursa ya kuwasilisha mada mbalimbali kwa njia ya maigizo, nyimbo na ushauri. Zifuatazo ni mada zilizo wasilishwa;

Umuhimu wa chakula mashuleni,Mada hii iliwasilishwa kwa njia ya igizo na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Shambalai, ikionesha umuhimu wa wanafunzi kupata chakula wawapo mashuleni ili kuongeza ufanisisi wa wanafunzi katika masomo yao.

Kushuka kwa uzalishaji wa mazao kipindi cha uviko-19, Mada hii iliwasilishwa na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Prince Claus ikionesha namna ambavyo Uviko-19 ulivyoathiri uzalishaji wa mazao ya chakula kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kwa ujumla.

Kujikinga na Uviko-19, Mada hii iliwasilishwa kwanjia ya wimbo na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Lushoto, wakizungumzia zaidi vijana kujikinga na ugonjwa hatari wa Uviko-19 ili kutunza na kuendeleza nguvu kazi ya taifa.

Umuhimu wa kula vya asili,Mada hii iliwasilishwa kwa njia ya igizo na wanafunzi kutoka shule ya sekondari Ubiri, ikionesha umuhimu wa matumizi sahihi ya vyakula. Matumizi ya kupindukia ya vyakula vitokavyo viwandani na vyakula vyenye mafuta mengi huathiri afya zetu kwa kiasi kikubwa pia hupelekea vifo kwasababu ya kemikali zitumikazo katika usindikaji wa vyakula hivyo.

                                                         The International Youth Day

World Youth Day was established by the United Nations in 1999 and was approved in 2000. The purpose of the day is to encourage the form of cultural and legal issues related to young people. World Youth Day is celebrated annually and 12th Aug is approved as opportunities for government and non-governmental orgaisations to bring young people together and guide them to discuss various issues that affect their lives. The celebrations involve concerts, workshops, cultural occasions, meetings and discussions to mention a few that are being conducted worldwide and usually attended by young people, elderly people, government officials, local authorities, youth-based organisations and community members at large.

YPM as one of youth-based organisation Tanzania which luckily got its registration on very 12th of Aug 2014 celebrated the day by gathering together young people at her head offices in Lushoto. Youth Peacemakers celebrated the International Youth Day by considering the theme of the day which is “CONSOLIDATION OF FOOD SYSTEMS IN MENTAL AND BODY HEALTH GROWTH FOR YOUNG PEOPLE” where by different government speakers, school students and volunteers cemented their discussion and presentation according to the theme.

The purpose of the event was to encourage young people to use natural foods for mental and body health growth. The young people had the opportunity to present various topics through drama and songs. The following topics were presented by different speakers during the gathering as follows;

The importance of food in School, this topic was presented through the drama by the students from Shambalai Secondary School, showing the importance of pupils to get food in schools so as to increase the activeness of their mind during studies hours.                                                                                                                   The decline in crop production duringCovid-19, This was presented by the students from Prince Claus Secondary school, showing how covid-19 affected food production from the family level to the nation level.                                                                                                                                                                    Fighting against Covid-19, this was presented through song by the students from Lushoto secondary school, leaving young people with a good message of protecting themselves from the risk of covid-19 so as to maintain and develop the national man power.                                                                                                       The importance of natural foods, this topic was presented through the drama by students from Ubiri secondary school, indicating the importance of maintaining proper eating habits. The students stressed that the excessive use of processed foods may affect young health largely, also it can cause diseases like cancer which might lead to deaths.

Finally, YPM presents gratitude to the Lushoto District Executive Director Miss. Ikupa Mwasyoge, the Lushoto District Educational officer at Primary School level, Shambalai, Lushoto, Ubiri and Prince Claus secondary school students who attended the event.

The Second Day of 3rd SADC Youth Forum

3rd SADC Youth Forum

Mkutano wa SADC unaohusisha vijana uliendelea kwa siku ya pili katika ofisi zetu za YPM Lushoto ulio hudhuriwa na vijjana 12 unaoendeshwa na Malawi kupitia mtandao wa Zoom.

Kwa siku hii ya pili vijana waliendelea kujifunza  mada zifuatazo;

 “Vyombo vya Habari na vijana” (Mchango wa vyombo vya Habari katika maendeleo endelevu ya vijana waliopo katika nchi za SADC)

 “Mchango wa vijana wa SADC katika kupambana na magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele (NTDS) na Malaria “(Kupanga mikakati ya kupambana na magonjwa ya kitropiko yasiyopewa kipaumbele na Malaria katika nchi za SADC)

“Jinsia na Maendeleo ya Wanawake” (Kufichua unyanyasaji wa kijinsia uliofanyika wakati wa Uviko 19 hadi sasa)

SADC meeting have proceeded with 12 YPM Youth at YPM Head Office in Lushoto which is hosted by Malawi via Zoom, in this second day of the meeting, the following topics have been addressed;

“Media and Youth round table” (Locating the role of media in sustainable Youth Development in SADC)

“SADC Youth task force on NTDs and Malaria”, (Setting a sustainable course to fight NTDs and Malaria in SADC: Call to Action)

“Gender and Women development” (Addressing gender-based violence during and post Covid-19)

3rd SADC Youth Forum

Around 12 YPM youth have gathered here at the YPM head office in Lushoto to attend 3rd Southern of Africa Development Community (SADC) meeting hosted in Malawi via Zoom. The theme of the meeting is “Blue and Green Economy for Sustainable Development” . During the first day of meeting the following topics have been addressed;

“Stop the Bleeding: Enhancing Domestics Resource Mobilization to Finance Youth Development (Bolstering SADC youth participation in global tax reforms to curb IFFs and improve finance for sustainable development in Africa”) and the other session was about Strategies to ensure Inclusive and Quality Education During Covid-19 Pandemic.

YOUTH AND EMPLOYMENT IN THE CONTEMPORARY WORLD

YPM attended a public lecture prepared by the University of Arusha on the topic of youth and employment in the contemporary world held at University of Arusha. The public lecture was hosted by the University of arusha administration lead by the Vice chancellor Professor Patrick Manu. The guest speaker was Honorable Humphrey Polepole a member of the Parliament of United republic of Tanzania and a Chairman of Parliamentary Standing Committee on Administration and Local Government in the Parliament of United republic of Tanzania.

Other stakeholders from national level (Tanzania Employment Services Agency under the Prime Minister’s Office Labor, Employment, Youth and People with Disability) and reginal level (the east African Community Youth Council) attended the event.

Group photo after the events/YPM

During the presentation Mr. Humphrey Polepole urged that, in Tanzania there is a low level of unemployment estimated to 2% to 6 % but there is a high level of underemployment and this is because firstly, the education system does not allow youth to have productivity in the employment secondly poor agriculture system which employs 75% of Tanzanians and  contributing to over 29% of the Growth Domestic Product thirdly, young people do not see the challenges facing the world as an opportunity to  them and  offer solutions through innovation ,creative thinking and  lastly the Government does not fully participate in the fourth added Hon. Polepole.  

Hon. Polepole further concluded that, the government shall modify the education system that will prepare well youth and provides support to the education institution so that they can produce desirable skills to meet the employment market demands. Not only that but also, the government shall participate and prepare youth effectively in the fourth industrial revolution.