Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa inayosumbua dunia. Hii nikutokana na kuambatana na majanga makubwa Kama vile ukame au mafuriko ambayo huhatarisha maisha ya mwanadamu hapa duniani. Katika jitihada za kupambana na changamoto hii, Ubalozi wa uholanzi nchini Tanzania uliandaa mkutano uliokutanisha takribani vijana 100 kutoka sehemu mbalimbali katika jengo la taasisi ya Alliance Françise jini Dar es salaam kwa lengo la kuwahamasisha vijana kuchukua jukumu la kuyalinda mazingira kwa vitendo ilikuifanya dunia kuwa sehemu salama kuishi.

Mkutano ulifunguliwa na salamu za ukaribisho kutoka kwa balozi wa Uholanzi nchini Tanzania na wazungumzaji rasmi walikua ni vijana wanaharakati wa kutetea mazingira na kila mmoja alieleza hadithi yake ambayo Ilikua na mguso wa namna yake tangu alipoanza harakati hadi aliposasa. Hadithi zao zilikua hamasa kubwa kwelikweli kiasi cha kumfanya kila kijana akiwa na ari ya kutaka kupanda miti Kama sehemu ya kuyalinda na kuyatunza mazingira.
Katika kipindi cha maswali na majibu ilibainika kuwa shauku ya kutaka kupunguza mabadiliko ya tabia ya nchi ni kubwa sana kuliko matendo yanayofanyika, hii nikutokana na kuwa na sera nzuri na elimu pia, lakini changamoto yake ni kwamba havimpi ulazima mwanamchi kulibeba jukumu la kuyalinda mazingira.
Makubaliano ni kwamba changamoto hii iendelee kuzungumzwa kukuza uelewa wa raia lakini lazima zitafutwe mbinu zitakazomlazimisha kila mmoja kutunza mazingira ama akiwa anataka au hataki kwakuwa hata katika familia unaweza kuandaa chakula kizuri kinachoweza kumfanya mtoto awe na afya tele lakini yeye akakataa kula. Hivyo lazima itafutwe mbinu alazimishwe kula ilianufaike na chakula kile. Vinginevyo mikutano ya namna hii itakosa nguvu kwanza itakuwa ikijadili tu na kuandaa mikakati mizuri lakini utekelezaji hakuna na changamoto itabaki palepale.
Kutoka Taasisi ya Vijana Waleta Amani Tanzania vijana 13 walipata nafasi ya kushiriki mkutano huo. Mbali na kukuza uelewa na hamasa kutoka kwa vijana wenzao walipata wasaa mzuri wa kutengeneza marafiki wapya kutoka taasisi mbalimbali zilizo hudhuria hivyo kuifanya familia ya Vijana Waleta Amani kutambulika na kuwa kubwa zaidi.
Climate change is a major challenge facing the world. This is due to the presence of major disasters such as droughts or floods that endanger human life on earth. In an effort to address this challenge, the Dutch Embassy in Tanzania organized a conference that brought together about 100 young people from various parts of the Alliance Françise building in Dar es Salaam with the aim of motivating young people to take responsibility for environmental protection to make the world a better place to live.
The meeting was opened with welcome greetings from the Dutch Ambassador to Tanzania and the official speakers were young activists and each told his own story which was very inspiring and have its kind of impact from the beginning to the present. Their stories very impressive that they made every young person want to plant trees as part of protecting and caring for the environment.
During the question-and-answer session it was found that the desire to reduce climate change is far greater than the actions taking place, this is due to having good policies and education as well, but the challenge is that they do not give citizens the responsibility to protect the environment.
The consensus is that this challenge should continue to be discussed to raise public awareness but strategies must be employed that will force everyone to take care of the environment whether they want it or not because even in the family you can prepare healthy food that can keep a child healthy but he or she refuses to eat. So a method must be employed to force him to eat in order to benefit from that food. Otherwise meetings of this nature will lack strength first will only discuss and devise good strategies but no implementation and challenges will remain the same.
From the YPM Tanzania 13 young people had the opportunity to participate in the conference. In addition to nurturing understanding and motivation from their peers, they also had the opportunity to make new friends from various attending Organization, thus making the YPM family big recognizable.