Trees Planting

Jitihada za kutunza Mazingira zinazofanywa na Youth Peace Makers Tanzania ikishikiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Maendeleo Endelevu ya Dunia hasa lengo namba 13 linalosema Kuchukua Hatua juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa zimezidi kupamba moto ambapo YPM imegawa miche ya miti kwa jamii katika ukanda wa tambarare Mkoa wa Tanga. Zoezi hili limesimamiwa na Kikundi Cha Kijamii Cha Huduma Ndogo za Fedha cha Mgombezi ambao ndio wasimamizi wa kitalu cha YPM kilichopo Mgombezi. YPM imegawa miche 200 kwa Shule ya Msingi  Mswaha, miche 250 kwa Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Fedha vya Handeni, Vikundi vya Komsala miche 60, Dumizi Mgombezi miche 100, Kanisa la Roma   Mgombezi miche 30,Misikiti ya Mgombezi miche 200 na Shule ya Msingi Mgambo miche 200. YPM inapenda kuwakumbusha kwamba miti hii inatolewa bure kabisa, na jukumu lako uliepokea huduma hii nikuhakikisha kuwa miti hiyo inatunzwa na  inakua iliiweze kukunufaisha wewe na jamii inayokuzunguka.

The tremendous efforts to protect the environment by Youth Peace Makers Tanzania have continued to bear fruits whereby YPM is actively participating in the implementation of Sustainable Development Goals (SDGs) in particular goal number 13 among other goals. The goal number 13 says “CLIMATE ACTION” which means taking action on Climate Change. In making sure that we tackle the challenge, YPM had distributed tree seedlings to communities in the lower land part of the Region of Tanga. The activity was supervised by the Community Microfinance Group of Mgombezi who take care of the YPM trees nursery at Mgombezi. YPM has distributed 200 trees to Mswaha Primary School, 250 trees to Handeni SIGs, 60 trees to SIGs at Komsala , 100 Trees to Duminzi Mgombezi, Roman Catholic  Church 30 trees, Mosques around Mgombezi 200 trees and 200 trees to Mgambo Primary School.

YPM would like to remind you that these trees are provided free of charge, and your responsibility when receiving this service is to ensure that the trees are cared for and grow so that it can benefit you and the community around you.

The International African Child Day

Today, June 16, the world celebrates the International Day of the African Child with the message “Implement the 2040 Agenda, for the Africa that Protect Children’s Rights”. In Lushoto district this ceremony took place in Yoghoi village where Government, Private and Government Officials came together to educate the community on the eradication of child abuse and violence. YPM Environment and Advocacy Officer Miss. Lidya Mshemu got a chance to talk to parents as well as children. Miss Mshemu, urged parents to reflect on this important day for children and the world at large and to see how they can work with various development partners and the Government to end child abuse and ensure that children get their rights. He added that YPM recognizes and fights for the rights of the child by launching a ‘Let Me Study Education is my Redeemer, conducting various dialogue and encouraging community to fight against Early Marriage and Early Pregnancy which has been a big challenge that have led to school drop out for many young girls. Not only that, but YPM has succeeded in contributing to the cost of health insurance for some vulnerable children in Lushoto District as well as distributing water containers for hand washing to schools to enable children to protect themselves from diarrhea and typhoid and improve their hygiene. All of this is to ensure that YPM is in support of the community development and enables children to fulfill their future dreams.As a parent, guardian, youth or development partner, let us work together to protect the African children as they are our treasure.

Yoghoi Primary School kids singing their poem in front of the Guest of Honor

Leo tarehe 16 ya mwezi Juni dunia inaazimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika yenye  ujumbe “Tutekeleze Ajenda 2040, kwa Afrika inayolinda Haki za mtoto”. Katika wilaya Lushoto maazimisho haya yamefanyika Katika kijiji cha Yoghoi ambapo Viongozi wa Serikali,Mashirika Binafsi na Yakiserikali wamejumuika kwapamoja ilikuelimisha jamii juu za kutokomeza vitendo vya kinyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto.Afisa Mazingira na Utetezizi wa YPM Miss. Lidya Mshemu alipata nafasi ya kuzungumza na wazazi pamoja na watoto. Miss Mshemu, aliwaasa wazazi kutafakari juu ya siku hii muhimu kwa watoto na dunia kwaujumla na kuona nijinsi gani wanweza kushirikiana na wadau mbalimbali wamaendeleo na Serikali ili kutokomeza ukatili kwa watoto na kuhakikisha kwamba watoto wanapata haki zao. Aliongeza kwa kusema kwamba, YPM inatambua na kupigania Haki za Mtoto kwa kuanzisha kampeni ya ”Niache nisome Elimu ndio Mkombozi wangu, Kuendesha majadiliano mbalimbali na kuhamasisha jamii kupiga vita Ndoa za Utotoni na Mimba za Utotoni. Si hivyo tu, lakini YPM imefanikiwa kuchangia gharama za bima ya Afya kwa baadhi ya Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu hapa Wilaya Lushoto pamoja na kusambaza ndoo za kunawia mikono mashuleni ili kuwezesha watoto kujikinga na magonjwa ya kuhara na typhoid. Yote haya nikuhakikisha kua YPM inakua msaada kwa jamii na kuwezesha watoto kutimiza ndoto zao.

IJA Peace Club performing short drama to educate the audience about Child rights and how they can be protect

Ukiwa Mzazi,Mlezi, Kijana au Mdau wa Maendeleo, tushirikiane kwa pamoja kumlinda mtoto wa Afrika kwani ndio hazina yetu.

SIGs Monitoring and Evaluation

Kuanzia tarehe 08 ya mwezi wa 06 hadi tarehe 10 ya mwezi Juni YPM imetembelea Vikundi Vya Kijamii Vya Huduma Ndogo za Fedha Halimashauri ya Bumbuli katika kijiji cha Muwao, Kabuku Wilayani Handeni, Tanga mjini pamoja na Duga Maforoni na Moa. Lengo kuu la ziara hiyo nikutatua changamoto mbalimbali zinazokubwa vikundi pamoja na kuwaelimisha na kuwahamasisha wanavikundi kusajili vikundi vyao. Zaidi ya yote Elimu ya Ujasiliamari ilitolewa kwa wanavikundi hao ili wana vikundi hao waweze kuchangamkia fursa mabalimbali za kiuchumi wanazokutana nazo.

From the 08th of the month of 06 to 10th of June YPM has visited the Community Small Financial Services Groups Bumbuli Council in Muwao village, Kabuku in Handeni District, Tanga town as well as Duga Maforoni and Moa. The main purpose of the visit is to address the various challenges facing groups as well as to educate and motivate group members to register their groups. Most of all, Entrepreneurship Education was provided to these group members to empower them to grab all economic opportunities with and outside their residence areas.

The World Environmental Day

Siku ya Mazingira Duniani

Tarehe 5 ya mwezi wa 6 kila mwaka dunia husherehekea siku ya Mazingira Duniani, siku hii ilianzishwa rasmi na Umoja wa Mataifa mwaka 1972 ikiwa na kusudi kubwa la kueleza changamoto mbalimbali zinazokuba mazinira yetu lakini pia kusaidia kuelimisha jamii juu ya mazingira,changamoto zinzokumba mazingira na njia gani zitumike ili kutunza mazingira.Kwa mwaka huu Siku ya mazingira duniani imeazimishwa nchini Pakistani,kitaifa imeazimishwa Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma halikadhirika kiwilaya imefanyika Kata ya Lushoto katika viwanja vya Nyerere Squire.Sikuu hii imebeba kauli mbiu inayosema “KUOKOA MFUMO WA IKOLOGIA” .Katika siku hii muhimu YPM imeshiriki kutuza mazingira kwa kugawa miti na kupanda miti zaidi ya mia tatu(300) katika vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha vya kata ya Ngulwi.Meneja miradi Bwan. Peter Jally akiambatana na Afisa Mazingira na Utetezi Bi.Lidya Mshemu pamoja na wafanya kazi wengine wa YPM wamehamasisha vikundi hivyo juu ya utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti lakini pia, kwakutumia nishati mbadala. Watumishi hao wa YPM walivieleza vikundi hivyo madhara yanayotokea kotokana utonzaji mbovu ma mazingira kama mabadiliko ya hali ya hewa yaliopelekea mvua nyingi kunyesha na kuharibu mazao pamoja na miundo mbinu kwa mwaka 2020.Baada ya hapo zoezi la upandaji miti liliendelea kwenye mashamba yao ambapo wanavikundi hao walielekezwa vipimo sahihi na naamna ya kupanda miti hiyo.

The World Environmental Day

On the 5th of June every year the world celebrates World Environment Day, this day was officially established by the United Nations in 1972 with the aim of highlighting the various challenges facing our environment but also helping to educate society about the environment. This year World Environment Day has been celebrated in Pakistan, national has been celebrated at the country’s Capital City in Dodoma and District level was celebrated at Lushoto ward on the Nyerere squire ground. On this important day, YPM has been involved in protecting the environment by donating trees and planting more than three hundred (300) trees to the Community Microfinance Groups (CMGs)of Ngulwi Ward in Lushoto District. The Program Manager Mr. Peter Jally accompanied by Environment and Advocacy Officer Ms. Lidya Mshemu along with other YPM staff members have encouraged the groups on environmental protection by planting trees but also by using renewable energy The YPM staff briefed the groups on the effects of poor weather and climate change, which led to heavy rains and crop failures as well as infrastructure in 2020. After that, tree planting continued on their farms where the group members were directed on the accurate measurements and on how to plant those trees better.

The National Torch of Freedom

Youth peace makers wakipata nafasi ya kishiriki siku ya mbio za mwenge ambapo mwenge ulipita wilayani Lushoto ili kukagua na kuzindua miradi mbali mbali ya kitaifa. Maadhimisho haya yaliongozwa na kiongozi wa Mbio za mwenge LT.Josephine P. Mwambashi, (Pichani no 3)ambapo pia alipata nafasi ya kupitia banda la YPM na kujifunza kuhusu shughuli zote zinazofanywa na taasisi yetu…

Youth Peace Makers got a chance to participate in the activities of National Torch where by the organization got a chance to talk about it’s activities with the leader of the event Lt.Josephine P. Mwambashi (Picture No 3).

CMGs Monitoring, Evaluation and Training

Taasisi ya YPM ikiongozwa na Meneja Miradi Mr. Peter Jally pamoja na wafanyakazi wengine wa YPM wametembelea Vikundi vya Kijamii vya Huduma Ndogo za Fedha (Community Microfinance Groups (CMGs). Vikundi vilivyotembelewa ni vya Mnazi pamoja na Mbaramo katika Wilaya Lushoto. Aidha, Meneja Miradi katika semina alioiendesha amewaeleza wanavikundi hao na kuwafafanulia juu ya sheria inayovitaka vikundi hivyo visajiliwe. Pamoja na hayo alisisitiza mshikamano na kufuata sheria,kanuni na taaratibu ambazo vikundi hivyo vimejiwekea ilikuhakikisha vinafikia malengo yao.

YPM led by Program Manager Mr. Peter Jally and other staff visited Community Microfinance Groups (CMGs) of Mnazi and Mbaramo in Lushoto District to see how the groups are doing but also to insists on the importance of registering their groups as the law requires. In addition, the Program Manager emphasized the groups to follow all the rules, regulations and procedures that the groups have set themselves to ensure that they achieve their goals.

YPM FORUM

Kutana na Youth Peace Makers Forum (YPMF) vijana kutoka Machame Health Institute ambao wanajishughulisha na harakati mbali mbali za kuhakikisha jamii inakuwa salama kimazingira na pia kwenye sekta ya usawa wa kijinsia.Forum hii inajihusisha sana na SDG no 10 Ambayo ni Climate Action pamoja na 17- Reduced inequalities chini ya mwamvuli wa Taasisi ya Youth Peace Tanzania.

Meet Youth Peace Makers Forum(YMPF), these are youth from Machame Health Institute that works hand in hand with Youth Peace Pakers Tanzania to make sure society gets all the help they need specially from the SDG goal no 17&10 that is Climate action and Reduced Inequality. YPM is very proud of this group and appreciate all the work they are doing to make sure the society is safe and gets all the knowledge they deseve.

IJA Peace Club

 IJA Peace Makers

There has been a very productive discussion with 18 youth from the Institute of Judicial Administration (IJA). The purposes were to discuss how the students would be able to collaborate with the YPM, choosing the leadership of the peace club where the Chairperson was elected to be Ms.  Mwanahamisi Sadick the secretary was appointed Mr. Rashid Mdee and the Disciplinary Officer was elected Mr. Josue Felician. Not only that, but the young people discussed how they will address various challenges such as pollution in Lushoto District as well as educate the community on recognizing the laws of Tanzania and becoming good citizens who know their rights and responsibilities. We are grateful that youth are self-aware and actively involved in activities that affect the future of their lives.

Kulikua na mazungumzo mazuri kati ya YPM na vijana 18 kutoka Chuo cha Uongozi  wa Mahakama (IJA). Madhumini yalikua kujadili jinsi wanafunzi  hao watakavyoweza kushirikiana na taasisi ya YPM,Kuchagua uongozi wa peace club ambapo Mwenyekiti alichaguliwa kua Bi. Mwanahamisi Sadick katibu akachaguliwa  Bwn.Rashid Mdee na Mtunza nidhamu alichaguliwa  Bwn. Josue Felician. Sio hivyo tu, bali vijana hao walijadili jinsi watakavyotatua changamoto mbalimbali kama uchafuzi wa mazingira katika Wilaya ya Lushoto pamoja na kuelimisha jamii juu ya kutambua sheria za Tanzania na kua raia wema wanaojua haki na wajibu wao. Tanashukuru kwamba vijana wanajitambua na kushiriki vyema katika shughuli zinazohusu muktakabali wa maisha yao.

Agribusiness

Leo YPM imetembelea wakulima wa viazi mviringo  wa Kwedeghe ambao ni wanavikundi vya kijamii vya  watoa huduma ndogo za kifedha. Dhumuni nikuwaunganisha wakulima hawa na soko ili waweze kuuza zao hili kwa urahisi ambapo YPM imemtafuta mfanya biashara ambaye yupo tayari kununua zao hilo kwa wakulima kwa bei nzuri.

Today YPM has visited the Kwedeghe potatoes growers who are members Community Microfinance Groups. The purpose is to connect these farmers with the market so that they can sell this crop easily. In addition to that, YPM has brought a trader who is willing to buy the potatoes from those farmers in good price.

Mdahalo

Leo taasisi ya YPM ilipata nafasi ya kushiriki katika mdahalo wa mawazo kati ya wanafunzi wa chuo cha mahakama cha IJA (Institute of Judicial Administration) na Chuo cha Ufundi Mabughai -Lushoto Mada ikiwa inasema “Je kuna usawa kati ya jinsia ya kike na jinsia ya kiume katika jamii inayokuzunguka” Upande wa kuunga mkono hoja walikuwa Chuo cha Maendeleo ya jamii na Ufundi na upande wa Kupinga hoja ikiwa ni Chuo Mungu ni mwema vijana wametupa ushirikiano mzuri sana wanachuo wa IJA pamoja na wa Mabughai! Thanks also to YPM crew kwa ushiriki na ushirikiano chanya! *#Youth Peacemakers Tanzania………..together we can!*