Mradi wa miti unaosimamiwa na vijana katika eneo la Kanisa la Lutherani umepiga hatua kubwa, licha ya changamoto ya ukame na uhitaji wa mbegu zaidi lakini vijana wameonyesha juhudi kubwa. Meneja wa YPM Bw. Peter Jally amewashauri kuongeza uzito katika upandaji wa miti ya matunda, miti ya mbao, na hata maua, kwa kuwa pia ni biashara yenye faida.
Katika hatua nyingine, wanafunzi wa shule za msingi Maforoni A & B walipata elimu muhimu kuhusu Utetezi, Mazingira, na Michezo, wakiongozwa na maafisa wa YPM. Mafanikio zaidi yameonekana kwa kuanzishwa kwa kitalu cha miti ambacho sasa kinasubiri mbegu ili miti iweze kupandwa kwenye viriba vilivyokwishaandaliwa.
Katika shule ya sekondari Zingibari, elimu kuhusu masuala ya Utetezi, Mazingira, na Michezo ilitolewa pia. Wanafunzi wameahidi kuunda Peace Club, itakayofuatilia masuala kama mimba za utotoni na kuendesha kampeni nyingine zinazoendeshwa na YPM kwa shule na jamii kwa ujumla.
Hii ni hatua kubwa kuelekea maendeleo ya kijamii kupitia juhudi za pamoja za vijana, walimu, na YPM.
#UtunzajiWaMazingira #PeaceClubs #YPM #MazingiraNaVijana #MichezoKwaMaendeleo #MazaoNaBiashara
Youth-led Tree Planting and Environmental Education Project
A youth-led tree-planting project at the Lutheran Church grounds is making great progress despite challenges like drought and a need for more seeds, the youth have shown remarkable dedication. The Manager encouraged them to prioritize fruit and timber trees and to consider flowers as they are also a profitable venture.
Meanwhile, students from Maforoni A & B primary schools received vital education on Advocacy, Environment, and Sports, facilitated by YPM program officers. Notable progress includes the establishment of a tree nursery, which is now awaiting seeds to plant in already-prepared planting bags.
At Zingibari Secondary School, the same education was delivered, and students pledged to form a Peace Club. This club will focus on addressing issues like teenage pregnancies and running other campaigns initiated and supported by YPM within their school and the broader community.
These initiatives reflect a significant step toward community development through collaborative efforts of youth, teachers, and YPM.
#EnvironmentalCare #PeaceClubs #YPM #YouthForEnvironment #SportsForDevelopment #AdvocacyAndChange