Bonanza la Vijana wa U13 na U20 Duga Maforoni

Bonanza la kuvutia lililoshirikisha jumla ya timu sita – mbili za U13 na nne za U20 – limefanyika katika viwanja vya Duga Maforoni.

Bonanza hili ni sehemu ya mradi wa pamoja kati ya CHRISC TANZANIA na YPM, likilenga kuwaandaa wataalamu wa michezo, hasa mpira wa miguu. Tayari hatua mbalimbali zimefanyika, ikiwemo:
✅ Kozi za makocha
✅ Mikutano ya wadau katika wilaya za Lushoto na Mkinga

Hadi sasa, makocha takribani 50 wameshiriki katika mafunzo haya, na matokeo yake yameanza kuonekana! Timu za vijana zimeanza kuundwa chini ya uongozi wa makocha hawa waliobobea.

Michezo ni msingi wa maendeleo ya vijana na jamii. Endelea kufuatilia kwa mengi zaidi kuhusu mradi huu.

#VijanaNaMichezo #CHRISC #YPM #U13 #U20 #SportsForDevelopment #MichezoKwaMaendeleo


U13 and U20 Youth Bonanza at Duga Maforoni
An exciting bonanza featuring six teams – two U13 and four U20 – took place at Duga Maforoni grounds.

This event is part of a joint project between CHRISC TANZANIA and YPM, aimed at developing sports experts, particularly in football. Key milestones achieved so far include:
✅ Coaching courses
✅ Stakeholder meetings in Lushoto and Mkinga districts

To date, approximately 50 coaches have participated in these trainings, and the results are already visible! Youth teams are now being formed under the leadership of these skilled coaches.

Sports are a cornerstone for youth and community development. Stay tuned for more updates on this impactful project.

#YouthInSports #CHRISC #YPM #U13 #U20 #SportsForDevelopment #YouthEmpowerment

Fainali ya Stop Poverty Cup Mkinga 2024

Timu ya Moa Stars imetawazwa kuwa mabingwa wa Stop Poverty Cup 2024 baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kijiru Stars

Mashindano ya mwaka huu yaliendeshwa kwa kauli mbiu ya “4, 4, 2”, ikisisitiza umuhimu wa mikopo inayotolewa na serikali kupitia Halmashauri kwa WANAWAKE, VIJANA, na WALEMAVU. Lengo kuu ni kuhamasisha vijana kujiunga katika vikundi, kubuni miradi, na kuandaa maandiko bora ya miradi ili kufanikisha upatikanaji wa mikopo hiyo.

Vijana, huu ni wakati wako! Weka malengo, buni miradi, na chukua hatua kwa maendeleo ya jamii na kujitegemea kiuchumi.

#StopPovertyCup2024 #Mkinga #MikopoKwaVijana #MikopoKwaWanawake #MikopoKwaWalemavu #VijanaNaMaendeleo


Stop Poverty Cup Mkinga 2024 Finals
Moa Stars were crowned champions of the Stop Poverty Cup 2024 after a 3-0 victory against Kijiru Stars

This year’s tournament was held under the theme “4, 4, 2”, highlighting government loans provided through councils for WOMEN, YOUTH, and PEOPLE WITH DISABILITIES. The goal was to encourage young people to form groups, create innovative projects, and write solid project proposals to qualify for these loans.

Young people, this is your time! Set goals, develop projects, and take action toward community development and financial independence.

#StopPovertyCup2024 #Mkinga #LoansForYouth #LoansForWomen #LoansForPWDs #YouthEmpowerment

Mradi wa Miti na Elimu ya Mazingira kwa Vijana

Mradi wa miti unaosimamiwa na vijana katika eneo la Kanisa la Lutherani umepiga hatua kubwa, licha ya changamoto ya ukame na uhitaji wa mbegu zaidi lakini vijana wameonyesha juhudi kubwa. Meneja wa YPM Bw. Peter Jally amewashauri kuongeza uzito katika upandaji wa miti ya matunda, miti ya mbao, na hata maua, kwa kuwa pia ni biashara yenye faida.

Katika hatua nyingine, wanafunzi wa shule za msingi Maforoni A & B walipata elimu muhimu kuhusu Utetezi, Mazingira, na Michezo, wakiongozwa na maafisa wa YPM. Mafanikio zaidi yameonekana kwa kuanzishwa kwa kitalu cha miti ambacho sasa kinasubiri mbegu ili miti iweze kupandwa kwenye viriba vilivyokwishaandaliwa.

Katika shule ya sekondari Zingibari, elimu kuhusu masuala ya Utetezi, Mazingira, na Michezo ilitolewa pia. Wanafunzi wameahidi kuunda Peace Club, itakayofuatilia masuala kama mimba za utotoni na kuendesha kampeni nyingine zinazoendeshwa na YPM kwa shule na jamii kwa ujumla.

Hii ni hatua kubwa kuelekea maendeleo ya kijamii kupitia juhudi za pamoja za vijana, walimu, na YPM.

#UtunzajiWaMazingira #PeaceClubs #YPM #MazingiraNaVijana #MichezoKwaMaendeleo #MazaoNaBiashara


Youth-led Tree Planting and Environmental Education Project
A youth-led tree-planting project at the Lutheran Church grounds is making great progress despite challenges like drought and a need for more seeds, the youth have shown remarkable dedication. The Manager encouraged them to prioritize fruit and timber trees and to consider flowers as they are also a profitable venture.

Meanwhile, students from Maforoni A & B primary schools received vital education on Advocacy, Environment, and Sports, facilitated by YPM program officers. Notable progress includes the establishment of a tree nursery, which is now awaiting seeds to plant in already-prepared planting bags.

At Zingibari Secondary School, the same education was delivered, and students pledged to form a Peace Club. This club will focus on addressing issues like teenage pregnancies and running other campaigns initiated and supported by YPM within their school and the broader community.

These initiatives reflect a significant step toward community development through collaborative efforts of youth, teachers, and YPM.

#EnvironmentalCare #PeaceClubs #YPM #YouthForEnvironment #SportsForDevelopment #AdvocacyAndChange