Mama vijana kutoka Wilaya ya Mkinga wamepatiwa mafunzo kuhusu umuhimu wa ujuzi na maarifa katika kufanya maamuzi sahihi yenye kujenga maisha yao, familia na jamii kwa ujumla.

Pia, zoezi la monitoring lilifanyika katika Kikundi cha Huduma Ndogo za Kifedha cha Lengo Letu, kilichopo Kijiru, kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya kikundi na kuimarisha jitihada za kuwawezesha wanakikundi kiuchumi.
Aidha, wawakilishi kutoka YPM walihudhuria mechi za Mkinga Stop Poverty Cup, zinazolenga kuelimisha jamii kupambana na umasikini pamoja na kuhamasisha jamii kuelewa na kutekeleza misingi ya utunzaji wa amani kupitia michezo.
Ujuzi, maarifa na maamuzi sahihi ni msingi wa kujenga jamii yenye fursa, amani na maendeleo.

#MkingaStopPovertyCup#StopPoverty#YoungMothers#EconomicEmpowerment#PeaceBuilding YPM SportsForDevelopment Mkinga


