DIGITAL EAST AFRICAN CUP
Kila mwaka Y Global na washarika wake huandaa mashindano ya michezo ya Afrika Mashariki ambayo hufanyika mkoani Kilimanjaro Tanzania. Mashindano hayo hushirikisha Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo mashirika yote huleta timu mbalimbali katika mashindano haya.
Mwaka huu kutokana na janga la Uviko 19 imekua vigumu kushiriki mashindano kama ilivyokua kawaida. Y Global na washarika wake wametumia njia mbadala yakufanya mashindano haya kwa njia ya mtandao, ambapo kulitolewa masomo na majadiliano tofauti tofauti kuhusu michezo,jinsi ya kujikinga na magonjwa mbali mbali ikiwemo Uviko 19, Ujasiriamali, Usimamizi wa miradi na Kuongeza michezo mipya katika mashindano.
Tukiwa kama msharika wa Y Global (Shirika la vijana waleta amani Tanzania) tuliandaa vijana 14 kutoka klabu ya amani ya vijana ya chuo cha Uongozi wa mahakama na vijana wanaojitolea, ambao walishiriki katika mashindano hayo kwa kujifunza na kujadili masomo yote yaliotolewa katika kipindi cha siku mbili kuanzia tarehe 24 Juni mpaka 25 Juni 2021.

Every year Y Global and its partners host an East African sports tournament which used to take place in the Kilimanjaro region of Tanzania. The tournament involves member states of the East African Community where all partners organization bring different teams to the competition.
This year due to the Covid 19 Pandemic it has been difficult to participate in the competition physically. Y Global and its partners have used alternative way by conducting online competitions whereby the presentation on variety sports related courses, how to protect ourselves from various diseases including Covid 19, Entrepreneurship, Project Management and Adding new games in competitions were taught and discussed through Zoom meeting.

As a partner of Y Global (Youth Peace Makers Tanzania) organized 14 young people from the Institute of Judiciary Administration Peace Club and Youth Peace Makers Volunteers were participated in this competition and learned all the lessons given in two days from the date. 24 June to 25 June 2021.